KLABU ya Yanga imevunja kambi ya maandalizi ya michuano mbalimbali ya msimu ujao baada ya wachezaji wake wengi kuitwa kwenye timu zao za taifa. Anaripoti Mintanga Hunda. TUDAC0 … (endelea).
Yanga ambayo ilitua nchini Morocco tarehe 16 Agosti mwaka huu, ilitarajiwa kuweka kambi kwa siku 12 lakini sasa imekaa kwa siku sita pekee.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa kwa umma na kudhibitishwa na Mkurugenzi wa Uwekezaji wa GSM Mhandisi Hersi Said, kikosi cha timu hiyo kitaanza safari ya kurejea jijini Dar es salaam leo mchana kupitia Dubai kutokea Morocco.
Said alisema timu hiyo itarejea kwa makundi ambapo baada ya kundi la kwanza linalotarajiwa kufika nchini kesho, kundi linalofuata litaanza safari siku chache zijazo.
Yanga inajiandaa na michuano mbalimbali ikiwamo kilele cha wiki ya wananchi ni tarehe 29 Agosti, 2021, mtanange wa ngao ya jamii tarehe 25 Septemba 2021, ambapo itamenyana na Simba kama ishara ya ufunguzi wa ligi kuu bara msimu wa 2021/2022.
Pia Yanga ambayo msimu huu itashiriki mashindano ya Klabu Bingwa barani Afrika, mechi za raundi ya kwanza zinatarajiwa kupigwa kati ya tarehe 10-12 Septemba mwaka huu na maruadiano ni kati ya tarehe 17-19 Septemba.
Asante sana kwa kutuhabarisha
Hongereni sana wananchi. Kazi kazi.
Pigeni kazi watani.
Rafiki yako,
Aliko Musa.
Mbobezi Kwenye Majengo.