Friday , 19 April 2024
Home Kitengo Michezo Yanga yatua Kagera
Michezo

Yanga yatua Kagera

Spread the love

KIKOSI cha Yanga kimetua kwenye Uwanja wa ndege wa Bukoba mapema hii leo asubuhi tayari kwa mchezo wa Ligi Kuu dhidi ya Kagera Sugar siku ya Jumamosi kwenye Uwanja wa Kaitaba. Anaripoti Mwandishi Wetu, Kagera … (endelea).

Yanga imeondoka na kikosi chake kamili baada ya kucheza mchezo wake wa kirafiki siku ya Jana dhidi ya Mlandege Fc uliofanyika kwenye Uwanja wa Azam Complex Chamazi nakufanikiwa kuibuka na ushindi wa mabao 2-0.

Mara baada ya kumalizika mchezo dhidi ya Kagera kikosi hiko kinatarajia kwenda mkoani Morogoro kuvaana na Mtibwa Sugar kwenye Uwanja wa Jamhuri.

Yanga mpaka sasa imecheza michezo miwili ya Ligi Kuu Tanzania Bara na kuibuka na pointi nne, mara baada ya kupata ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Mbeya City na kwenda sare ya bao 1-1 mbele ya Tanzania Prisons.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Michezo

Leo ni leo nani kutinga nusu fainali UEFA?

Spread the love HATIMAYE Jumanne ya UEFA imefika ambapo leo hii michezo...

Michezo

Anza Jumatatu yako na Meridianbet

Spread the love  IKIWA ni siku nyingine mpya kabisa ya Jumatatu baadhi...

Habari MchanganyikoMichezo

NBC, Yanga wazindua kadi  za kimataifa za uanachama

Spread the loveBenki ya Taifa ya Biashara (NBC) kwa kushirikiana na Klabu...

Michezo

TFF, Amrouche ngoma nzito

Spread the loveVIPENGELE vya mkataba wa kazi aliotia saini Kocha Mkuu wa...

error: Content is protected !!