Tuesday , 23 April 2024
Home Kitengo Michezo Yanga yatoa kipigo cha ‘mbwa koko’, yajichimbia kileleni
Michezo

Yanga yatoa kipigo cha ‘mbwa koko’, yajichimbia kileleni

Deus Kaseke
Spread the love

MABINGWA wa kihistoria nchini Tanzania, Yanga ya jijini Dar es Salaam, wameendelea kujikusanyia pointi katika michezo ya Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara (VPL) 2020/21 kwa kutoa kipigo kikubwa kwa Mwandui FC cha 5-0. Anaripoti Kelvin Mwaipungu, Dar es Salaam … (endelea).

Yanga imeibuka na ushindi huo leo Jumamosi tarehe 12 Desemba 2020 katika Uwanja wa CCM Kambarage mkoani Shinyanga, ukiwa ni ushindi wa kwanza mkubwa kuupata tangu kuanza kwa ligi hiyo huku ikiwa haijapoteza mchezo wowote.

Ulikuwa mchezo ambao Yanga iliutawala kuanzia mwanzo hadi mwisho huku ikiwachukua dakika sita za kipindi cha kwanza kuandika bao lililofungwa na Deus Kaseke akiunganisha pasi nzuri iliyopigwa na Sogne Yacuba.

Yanga waliendelea kuliandama lango la Mwandui inayoshika nafasi ya 17 kati ya 18 ya msimamo wa Ligi Kuu na dakika ya 13, Yacuba akaiandikia bao la pili na dakika ya 48, Yacuba ambaye ni raina wa Bukuna Faso akaifungia la tatu.

Yacuba amefikisha magoli matatu ndani ya msimu mmoja wa ligi kuu.

Wakati shangwe zikiendelea kutawala uwanjani hapo kwa ushindi huo mkubwa, kiungo mshambuliaji Tuisila Kisinda, akaiandikia goli la nne dakika ya 56.

Dakika ya 70, beki kisiki wa Yanga, Lamie Moro aliwaandikia goli la tano, vijana wa Jangwani na kuibua shangwe uwanjani hapo hasa ikizingatiwa, Yanga ilikuwa ikipata ushindi kiduchu wa goli moja katika michezo kadhaa iliyopita.

Ushindi huo, umewafanya Yanga kufikisha pointi 37 ikiwa imecheza michezo 15 ikifuatiwa na Azam FC iliyocheza michezo 14 ikiwa na pointi 27 na Simba ina pointi 26 ikiwa imeshuka ndimbani mara 12.

Simba inashuka kesho Jumapili Uwanja wa Sokoine jijini Mbeya kucheza na Mbeya City.

Kocha wa Mwandui FC, Khalid Adam amesema, ukianza kupoteza mfululizo na ukiruhusu goli la mapema unapoteza uelekeo “tunaendelea kujipanga ili tuendelee kufanya vizuri.”

Amesema, anakusudia kufanya mabadiliko katika kikosi chake ikiwemo kuongeza wachezaji “kwani hawa wachezaji vijana hawawezi kunipa matokeo mazuri.”

Kwa upande wake Kocha wa Yanga, Cedrick Kaze amefurahishwa na mchezo huo huku akigusia suala la kuongeza wachezaji atazungumza kwanza na viongozi ili kuona nini wafanye “na tutaangalia vizuri, nafasi gani tunahitaji mchezaji na kama hakuna tutaendelea kutumia wale wale.”

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Michezo

Arsenal dhidi ya Chelsea ngoma nzito leo EPL

Spread the love  Leo kutakua na mchezo mkali sana pale kwenye ligi...

Habari MchanganyikoMichezo

NBC yanogesha Derby Kariakoo, Aziz Ki aibuka mchezaji bora Machi

Spread the loveBenki ya Taifa ya Biashara (NBC) ambayo ni mdhamini Mkuu...

Michezo

Ujanja ni kubeti na Meridianbet

Spread the love  JUMAPILI ya leo imekaa kihela hela sana ndani ya...

Michezo

Anza Jumamosi yako na mkwanja wa Meridianbet

Spread the loveJumamosi ya leo ODDS zimekaa kijanja sana ndani ya Meridianbet...

error: Content is protected !!