May 27, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Yanga yatangulia fainali, yazisubiri Simba au Azam

Spread the love

 

GOLI pekee ya mshambuliaji wa kimataifa kutoka Ghana wa Yanga ya Dar es Salaam, Yacouba Sogne, limeipeleka fainali ya michuano ya Azam Sports Federation Cup (ASFC). Anaripoti Kelvin Mwaipungu, Dar es Salaam … (endelea).

Yacouba ametupia goli hilo kwa shuti kali dakika ya 22, akipokea basi safi kutoka kwa kiungo mahiri, Feisal Salum.

Mchezo huo wa nusu fainali ya kwanza ya ASFC, imechezwa leo Ijumaa, tarehe 25 Juni 2021, katika Uwanja wa Ali Hassan Mwinyi, Mkoa wa Tabora.

Mshambuliaji wa Yanga, Yacouba Sogne akishangilia bao lake

Ulikuwa mchezo wa kushambuliana kwa zamani ambapo Yanga ilikuwa ikishambulia na Biashara wakijibu mapigo na kuufanya kuwa mchezo wa kuvutia kwa mashabiki waliojitokeza kwa wingi uwanjani hapo.

Yanga itaumana fainali na mshindi kati ya Azam FC na mabingwa watetezi wa kombe hilo, Simba katika nusu fainali ya pili, itakayopigwa kesho Jumamosi, kuanzia saa 9:30 alasiri, Uwanja wa Majimaji, Songea mkoa wa Ruvuma.

error: Content is protected !!