December 3, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Yanga yatamba mbele ya Kagera

Spread the love

KLABU ya soka ya Yanga imefanikiwa kuibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi Kagera Sugar kwenye mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara uliopigwa kwenye dimba la Kaitaba mkoani Kagera. Anaripoti Kelvin Mwaipungu, Dar es Salaam … (endelea).

Bao la Yanga kwenye mchezo huo lilifungwa na kiungo raia wa Congo, Mukoko Tunombe dakika ya 71’ baada ya kuunganisha pasi kutoka kwa Tuisila Kisinda.

Baada ya ushindi huo Yanga itakuwa imefikisha pointi saba kwa kushinda michezo miwili na kutoka sare mchezo mmoja.

Kwa upande wa Kagera Sugar wao watakuwa wameanza vibaya ligi hiyo mara baada ya kucheza michezo mitatu, wakipoteza michezo miwili na kwenda sare mechi moja na hivyo kufanya kuendelea kusalia na pointi moja.

Kufuatia ushindi huo Yanga itasafiri kuelekea mkoani Morogoro kucheza mchezo ujao wa ligi dhidi ya Mtibwa Sugar kwenye Uwanja wa Jamhuri siku ya tarehe 27 september 2020.

error: Content is protected !!