August 13, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Yanga yasonga mbele Ligi ya Mabingwa Afrika

Spread the love

[pullquote][/pullquote]PAMOJA na klabu ya Yanga kushindwa kutamba katika Uwanja wa nyumbani kwa kulazimishwa rase ya bao 1-1 dhidi ya APR ya Rwanda lakini wamesonga mbele katika Ligi ya Mabingwa Afrika, anaandika Kelvin Mwaipungu.

Yanga imesonga mbele katika michuano hiyo kwa jumla ya mabao 3-2, kutokana na mtaji wa ushindi wa mabao 2-1 waliopata katika mchezo wa kwanza uliocheza wiki iliyopita jijini Kigali.

Katika mchezo wa leo uliofanyika kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam, APR iliyokuwa ya kwanza kupata bao dakika ya tatu, lililofungwa na Fiston Nkinzingabo akiunganisha krosi ya Rutanga Eric.

Yanga walisawazisha bao lao kupitia kwa Donald Ngoma dakika ya 28, bao lililoduma mpaka mwisho wa mchezo huo na kufanya matokeo yawe 1-1.

error: Content is protected !!