January 19, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Yanga yarudi kileleni, Azam yabanwa na Ruvu

Simon Msuva akishangilia bao lake sambamba na mshambuliaji mwenzake, Mrisho Ngassa

Spread the love

USHINDI wa mabao 3-0 ulioipata Yanga dhidi ya Tanzania Prisons, umeifanya timu hiyo ikae kileleni mwa msimamo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara.

Yanga ambao imevuna ushindi huo katika mchezo uliochezwa kwenye Uwanja wa Sokoine jijini Mbeya, imefikisha pointi 28 huku wapinzani wao waliokuwa wanashindania nafasi hiyo, timu ya Azam FC ikikubali kuwapisha kileleni kwa kukubali kugawana pointi na Ruvu Shooting.

Azam iliyokuwa ugenini kwenye Uwanja wa Mabatini mjini Mlandizi, Pwani ilishindwa kupata pointi tatu muhimu katika uwanja huyo baada ya mechi hiyo kumalizika kwa suluhu.

Mabao ya Yanga katika mchezo huo yalifungwa na Simon Msuva aliyefunga mawili na moja Prisons walijifungwa baada ya beki kutaka kuokoa shuti la Andrey Coutinho ambalo lilikuwa linaelekea golini.

 

error: Content is protected !!