May 20, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Yanga yapotea Tanga, yakubali kichapo cha mabao 2-1

Spread the love

 

BAO la dakika ya 85 lilofungwa na Mudathir Abdallah lilitosha kuipatia ushindi wa mabao 2-1, timu ya Coastal Union dhidi ya Yanga kwenye mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara. Anaripoti Kelvin Mwaipungu, Dar es Salaam … (endelea).

Baada ya kukubali kipigo hiko Yanga imepoteza mchezo kwa mara ya kwanza kwenye Ligi Kuu Tanzania Bara mara baada ya kucheza michezo.

Coastal Union walikuwa wa kwanza kupata bao kwenye dakika ya 1o ya mchezo na baadae Tuisila Kisinda kusawazisha bao hilo dakika ya 37 na kufanya timu hizo kwenda mapumziko zikiwa zimefungana bao bao 1-1.

Kipindi cha pili kilianza kwa timu zote kushambuliana na Coastal Union kuandika bao la pili kupitia kwa Mudathir mara baada ya kuingia dakika chache akitokea benchi.

Mara baada ya mchezo huo kukamilika kocha wa Yanga, Cedric Kaze alieleza kuwa baada ya kushindwa kufunga penalti waliopata dakika ya saba kwenye mchezo, wenzao walijitahidi kucheza vizuri na kupata bao.

“Tuliposhindwa penalti na kufungwa bao la kwanza, tulijitahidi kubaki katika mchezo lakini wenzetu wamejitahidi kucheza vizuri maeneo mengi,” alisema Kaze.

Aidha Kaze pia aliongezea kuawa amekubali matokeo hayo na hana kisingizio na ataenda kujipanga kwa ajili ya mchezo ujao.

“Hatuna kisingizo, ni kwenda kujipanga tu kwa mchezo ujao, huu ni mchezo wa kwanza tunapoteza na hakuna haja ya kumtupia lawama mchezaji huyu au yule na Jumapili tunamechi nyingine,” aliongezea kocha huyo.

error: Content is protected !!