July 6, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Yanga yaiwahi Simba Kigoma, yapokelewa kwa shangwe

Wachezaji wa Yanga wakiwasili Kigoma

Spread the love

 

KIKOSI cha klabu ya Yanga kimetua rasmi mkoani Kigoma, kwa ajili ya mchezo wa fainali wa Kombe la Shirikisho (FA) dhidi ya watani wao Simba. Anaripoti Kelvin Mwaipungu, Kigoma … (endelea).

Mchezo huo utapigwa kwenye Uwanja wa Lake Tanganyika tarehe 25 Julai, majira ya saa 1o kamili jioni.

Yanga wamewasili Kigoma majira ya saa 1:15, kwenye Uwanja wa ndege wa Kigoma, kupitia Shirika la Ndege la Air Tanzania.

Baada ya kuwasili hapo kikosi hiko kilipokelewa na viongozi wa Yanga wakiongozwa na Kaimu Katibu Mkuu, Haji Mfikilwa, ambaye alitangulia Kigoma.

Ilipofika majira ya saa 1:35, msafara wa kikosi hiko ulitoka uwanjani hapo, huku ukilakiwa na mashabiki wao waliojitokeza kwa wingi na kuuzunguka mji wa Kigoma mpaka kuelekea Hotel ya Mwitongo ambapo kikosi hiko kimefikia hapo.

Kikosi hiko cha Yanga baadaye kitafanya mazoezi kwenye Kiwanja cha chuo cha Hali ya Hewa, Kigoma.

error: Content is protected !!