July 6, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Yanga yapita mlango mdogo, wagoma kuingia vyumbani

Spread the love

 

Katika hali ya kustajabisha, kwenye mchezo watani wa jadi kati ya Simba na Yanga, kikosi cha klabu ya Yanga ambao walikuwa wageni kwenye mchezo huo wa Ligi Kuu Tanzania Bara, hakikutumia geti kubwa kuingia uwanjani hapo. Anaripoti Kelvin Mwaipungu…(endelea)

Mchezo huo ambao umemalizika kwa Yanga kuibuka na ushindi wa bao 1-0, lilifungwa na kiungo wake Zawadi Mauya kwenye dakika 11 ya mchezo.

Yanga walifika Uwanjani hapo majiya ya saa 9 mchana na kuamua kupitisha gari lao, kwenye geti la Uwanja mdogo wa Uhuru kinyume na utaratibu wa kanuni za mashindano.

Kikosi hiko hakikuishia kufanya hivyo bali mara baada ya wachezaji kushuka kwenye gari hawakuingia kwenye vyumba vya kubadilishia nguo vilivyopangwa na kuamua kukaa nje ya vyumba hivyo.

Pia kikosi hiko, hakikutumia mlango mkubwa wa kuingia Uwanjani sehemu ya kuchezea kwa ajili ya kupasha misuli moto kabla ya mchezo kuanza.

Simba ndio waliokuwa wa kwanza kuingia uwanjani hapo kupasha misuli moto, kwa kutumia mlango wa siku zote, Yanga wao hawakufanya hivyo waliamua kutumia mlango wa pembeni kuingia eneo la kuchezea kupasha misuli moto kinyume na uataratibu.

error: Content is protected !!