Friday , 3 February 2023
Home Kitengo Michezo Yanga yampata mrithi wa Shikalo
MichezoTangulizi

Yanga yampata mrithi wa Shikalo

Djiugui Diarra
Spread the love

 

KLABU ya soka ya Yanga, imekamilisha usajili wa mlinda mlango Djigui Diarra, kutoka nchini Mali ambaye ameingia mkataba wa miaka miwili na timu hiyo. Anaripoti Kelvin Mwaipungu.

Mlinda mlango huyo anakuja kuchukua nafasi ya Farouk Shikalo, ambaye mkataba wake na klabu ya Yanga umefikia mwisho mara baada ya kuhudumu katika kipindi cha miaka miwili.

Shikalo alijiunga na Yanga, kwenye msimu wa 2019, akitokea kwenye klabu ya Bandari inayocheza Ligi Kuu nchini Kenya, lakini hakuawa na wakati mzuri wa kupata nafasi mbele ya Metacha Mnata na kuhesabika kama mlinda mlango namba mbili.

Diarra alifika jana jijini Dar es Salaam, na kutambulishwa hii leo, kuelekea msimu ujao wa mashindano, ambapo klabu ya Yanga itashikili michuano ya kimataifa.

Kipa huyo amepata mafanikio makubwa kwenye Ligi ya nchini Mali, akiwa na klabu ya Stade De Malien mara baada ya kushinda taji la Ligi Kuu nchini humo mara tano.

Aidha Diarra amefanikiwa tena kushinda mataji matatu ya kombe la FA, na mataji mawili ya kombe la Malian.

Mlinda malango huyo ambaye pia alifanikiwa kuwa katika kikosi cha timu ya Taifa ya Mali kwenye michuano ya kombe la mataifa Afrika kwa wachezaji wa ndani  2016 na 2021, na pia msimu uliopita alichaguliwa kuwa mchezaji bora wa Ligi hiyo ya nchini kwao.