MABINGWA wa Kihistoria nchini Tanzania, Yanga ya Dar es Salaam, imetoa salamu za rambirambi, kufuatia kifo cha Kenneth Kaunda, Rais wa kwanza wa Zambia. Anaripoti Kelvein Mwaipungu, Dar es Salaam … (endelea).
Kaunda (97), alifikwa na mauti jana Alhamisi, tarehe 17 Juni 2021, katika moja ya hospitali mjini Lusaka, Zambia alipokuwa akipatiwa matibabu.
Tangu kutokea kwa kifo hicho, salamu mbalimbali zimeendelea kutolewa ikiwemo Klabu ya Yanga ambayo uwanja wake wa mazoezi ulipo makao makuu, unatitwa Kaunda, rais huyo aliyoongoza Zambia kwa miaka 27 kuanzia 1964 hadi 1991.
“Salama za Rambirambi. Pumzika kwa amani Rais wa kwanza na Muasisi wa Taifa la Zambia Hayati Kenneth Kaunda.”
Salama za Rambirambi
Pumzika kwa amani Rais wa kwanza na Muasisi wa Taifa la Zambia Hayati Kenneth Kaunda pic.twitter.com/9bk4HvqKUZ
— Young Africans SC (@yangasc1935) June 18, 2021
“Klabu ya Yanga SC itaendelea kumkumbuka na kumuenzi Hayati Keneth Kaunda kwa kuhakikisha Uwanja wa Kaunda uliopo Makao Makuu ya Klabu, Jangwani unaendelezwa ikiwa ni sehemu muhimu ya kumbukumbu yake katika Historia ya Klabu yetu,” imeandika Yanga katika akaunti zake za kijamii
Hata hivyo, kwa sasa Uwanja huo wa Kaunda, haufanyi kazi, kwani kuna vifusi vimewekwa kwa kipindi kirefu kwa kile kinachosubiriwa kufanyiwa ukarabati mkubwa ili kuuwezesha kutumika.
Mara kadhaa, uwanja huo, umekuwa ukijaa maji pindi mvua inaponyesha kutokana na kuwa bondeni.
Leave a comment