Thursday , 30 March 2023
Home Kitengo Michezo Yanga yamfungia Metacha, mwenyewe aomba radhi
MichezoTangulizi

Yanga yamfungia Metacha, mwenyewe aomba radhi

Spread the love

 

MARA baada ya uongozi wa klabu ya Yanga kumfungia mlinda mlango wake Metacha Mnata, kwa kosa la utovu wa nidhamu, mchezaji huyo muda mchache baadae aliomba radhi kwa kufanya kitendo kisicho cha kiungwana. Anaripoti Kelvin Mwaipungu…(endelea)

Mlinda mlango huyo alifungiwa na uongozi wa klabu hiyo, kufuatia kuonesha ishara ya kidole kwa mashabiki wa klabu hiyo ambao walikuwa wanamzomea mara baada ya mpira kumalizika, kwa kuamini kuwa amefungwa bao la kizembe kwenye dakika ya 81, lililofungwa na kilomi.

Baada ya kumalizika kwa mchezo huo ambao Yanga waliibuka na ushindi wa mabao 3-2, uongozi huo ulitoa taarifa kwa umma ya kumsimamisha mchezaji huyo kwa muda usiojulikana na kesi yake kupelekwa kwenuye kamati ya maadili ya klabu hiyo.

Leo majira ya saa nane mchana, mchezaji huyo kupitia ukurasa wake wa Instagram aliomba radhi mashabiki, uongozi pamoja na wachezaji wa klabu hiyo, kwa kitendo kisicho cha kiungwana alichokifanya kwenye mchezo wa jana.

Metacha aliandika kuwa tukio lile halikuwa la kiungwana hivyo anajutia makossa yake na yeye kama mchezaji anapaswa kuwa mfano bora.

“Nikiri hakikuwa kitendo cha kiungwana hivyo najutia makosa niliyoyafanya. Mimi kama mchezaji wa Yanga na Timu ya Taifa napaswa kuwa mfano mzuri siku zote mbele za watoto na wanaotamani kuwa kama mimi na watu ambao aidha walikuwepo kiwanjani au waliona mechi kupitia Televisheni majumbani kwao.” Aliandika Metacha

Hiii ni mara ya pili kwa mchezaji huyo katika kipindi cha mwezio mmoja Metacha kushutmiwa na makossa ya utovu wa nidhamu ndani ya klabu ya Yanga.

Wakati timu hiyo ilipokwenda Shinyanga kwenye mchezo wa robo fainaliwa michuano ya kombe la Shirikisho (FA) dhidi ya MwaduI FC, mchezaji huyo alirudishwa Dar es Salaam na kocha Nasreddine Nabi kwa kosa la utovu wa nidhamu.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Michezo

TANROADS wawataka watumishi wazingatie michezo kazini

Spread the love  WAKALA wa barabara Tanzania (TANROADS) imesema michezo inapaswa kuzingatiwa...

Michezo

Yanga: Fedha za Rais Samia zinaleta ari kubwa

Spread the loveUONGOZI wa klabu ya Yanga, umesema fedha zinazotolewa na Rais...

Michezo

Simba Sc. yamvulia kofia Rais Samia, yamuahidi makubwa dhidi ya Horoya

Spread the loveWAKATI timu ya Simba ikiibuka na ushindi wa bao 3-0...

Habari MchanganyikoTangulizi

Rais Samia ampandisha cheo RPC wa Dar

Spread the loveMKUU wa Jeshi la Polisi nchini (IGP), Camillus Wambura, amesema...

error: Content is protected !!