July 6, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Yanga yalamba dili la bilioni 41

Spread the love

 

KLABU ya soka ya Yanga, imeingia mktaba wenye thamani ya shilini 41 bilioni, katika kipindi cha miaka 1o na kampuni ya Azam Media kwa ajili ya maudhui na kipindi cha Yanga TV. Anaripoti Kelvin Mwaipungu…(endelea)

Mkataba huo umesainiwa hii leo tarehe 8 Julai 2021, jijini Dar es Salaam, ambapo upande wa Yanga uliwakilishwa na mwenyekiti wa klabu hiyo, Dk. Mshindo Msolla huku Azam Media ikiwakilishwa na Tido Mhando ambaye ni Mkurugezni mtendaji wa kampuni hiyo.

Katika mkataba huo, klabu ya Yanga itajinyakulia kiasi cha milioni 200 kila mwezi, na itapa shilingi 3 bilioni kuanzia msimu ujao kama ikimaliza katika nafasi mbili za juu.

Kiwango hiko cha mwezi kitakuwa kinapanda kila msimu, kwa kuongezeka kiasi cha pesa.

error: Content is protected !!