Saturday , 15 June 2024
Home Kitengo Michezo Yanga yalaani kufanyiwa vurugu mashabiki wa Simba
Michezo

Yanga yalaani kufanyiwa vurugu mashabiki wa Simba

Mashabiki wa Yanga
Spread the love

KLABU ya soka ya Yanga imelaani vikali kitendo cha mashabiki wao kuwafanyia vurugu mashabiki wa klabu ya Simba kwenye mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara dhidi ya Mtibwa uliochezwa kwenye Uwanja wa Jamhuri mkoani Morogoro. Anaripoti Kelvin Mwaipungu, Dar es Salaam … (endelea).

Katika taarifa yao uongozi wa klabu ya Yanga unalaani tabia hiyo kutoka kwa mashabiki wao inayojengeka na kuvitaka vyombo vya ulinzi kuchunguza na kuchukua hatua kwa wale wote watakaobainika.

Tukio la aina hiyo litakuwa kwa mara ya pili kwa msimu kwa mashabiki wa klabu ya Yanga kuwafanyia fujo mashabiki wa Simba kwenye michezo mbalimbali.

Ikumbukwe katika kilele cha siku ya tamasha la wiki ya mwananchi lililofanyika 30 Agosti, 2020. kulitokea tukio la aina hii ambapo baadhi ya mashabiki wa Yanga walionekana kumchania jezi shabiki wa samba aliyefika kiwanjani kuangalia mchezo wa kirafiki kati ya Yanga na Aigle noir ya nchini Burundi.

Uongozi wa klabu hiyo pia umeendelea kusisitiza kuwa mchezo wa mpira wa miguu ni mchezo wa furaha na sio uadui kwani upinzani wao na Simba unataokana na utani wao wa jadi na sio uhasama.

Katika mchezo huo Yanga ilifanikiwa kuibuka na ushindi wa bao 1-0 mbele ya Mtibwa na kujipatia pointi tatu na kufikisha alama 10 sawa na Simba wakitofautiana magoli ya kufungwa na kushinda.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Michezo

Jumamosi ya leo ni ya pesa na EURO hapa Meridianbet

Spread the love  Baada ya jana kushuhudia mechi kali ya ufunguzi wa...

Michezo

Serikali yaondoa kodi vifaa vya ‘VAR’

Spread the love  SERIKALI ya Tanzania kupitia Waziri wa Fedha Dk. Mwigulu...

Michezo

Leo Tanzania ipo dimbani beti na Meridianbet

Spread the love  Mechi nyingi za kufuzu Kombe la Dunia kwa Afrika...

Michezo

Meridianbet inakwambia beti mechi spesho za EURO sasa

Spread the love Wakali wa ubashiri Tanzania Meridianbet wamekuja na Spesho ODDS...

error: Content is protected !!