UONGOZI wa klabu ya Yanga umeamua kukanusha taarifa ya kuondoka kwa kocha wao Mkuu, Mohamed Nabi mara baada ya kuenea tetesi za kuachana nae. Anaripoti Kelvin Mwaipungu…(endelea)
Kupitia …. Ya klabu hiyo walimnukuu mtendaji mkuu wa klabu hiyo Andre Mtine, ambaye aliwataka mashabiki na wanachama wa klabu hiyo kupata taarifa sahihi kwenye kurasa rasmi za klabu kwenye mitandao ya kijamii.
“Niwaombe mashabiki na wanachama wetu kuwa na utaratibu wa kufuatilia taarifa za klabu yetu kutoka kwenye vyanzo vyetu vya habari.” Alinukuliwa mtendaji huyo
Sintofahamu hiyo juu ya klabu ya Yanga kuachana na kocha huyo, ilibuka mapema siku ya leo huku sababu tofauti tofauti zikielezwa.
Taarifa za kocha huyo kutakan kufungashiwa virago zilianza kuenea mara baada ya Yanga kuondolewa kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Al Hilal ya nchini Sudan.
Licha ya kutolewa huko lakini klabu hiyo, ilipata nafasi ya kudondokea kwenye michuano ya kombe la Shirikisho barani Afrika, ambapo wananafasi ya kufuzu hatua ya makundi kama wakifanikiwa kuwaondosha Club Africain ya nchini Tunisia.
Pamoja na sintofahamu hiyo, kocha huyo hii leo alijitokeza mbele ya waandishi wa habari kuelezea maandalizi ya kikosi chake, kuelekea mchezo ujao wa Ligi Kuu Tanzania Bara dhidi ya Kmc.
Mchezo huo utapigwa kesho tarehe 26 Oktoba 2022, majira ya saa 1 usiku kwenye dimba la Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam.
Nabi alisema kuwa kwa sasa ratiba inaonekana kuwa ngumu mbele yao, lakini bado malengo yao ya kuchukua alama tatu kwenye mchezo huo wa leo bado yapo palepale.
“Tunafahamu kuwa ratiba yetu ni ngumu, tunafanya kila jitihada kwendana na uhalisia unaotukabili kwa sasa. Tuna mechi ngumu mbele yetu na huo ndio ukweli ambao tunapaswa kupambana nao. Sio suala la nani atacheza ni suala la alama tatu” alisema Nabi
Leave a comment