November 29, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Yanga yajikita kileleni, yampiga Ruvu tatu

Spread the love

 

 USHINDI wa mabao 3-1, dhidi ya Ruvu Shooting umzidi kuifanya klabu ya Yanga, kujichimbia kileleni kwenye msimamo wa Ligi Kuu Tanzania Bara wakiwa na pointi 15. Anaripoti Kelvin Mwaipungu…(endelea)

Mchezo huo ulipigwa hii leo, tarehe 2, novemba 2021kwenye dimba la Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam.

Yanga ambao walikuwa wenyeji wa mchezo huo, walianza kwa kuruhusu bao mapema kipindi cha kwanza kupitia kwa Shabani Msala dakika ya 9’ na kisha Feisal Salum alifanikiwa kuisawazishia Yanga bao hilo dakika ya 33’ na kufanya mpira kwenda mapumziko wakiwa wamefungana bao 1-1.

Kipindi cha pili kilipo rejea, Shabani Djuma alifanikiwa kuindikia Yanga bao la pili kwa njia ya mkwaju wa penati kwenye dakika ya 48 ya mchezo.

Dakika 22’ baadae, Mukoko Tonombe ambaye leo aliingia kuchukua nafasi ya Khalid Aucho ambaye hakuwa sehemu ya mchezo huo kutokana na kupata majeraha aliandikia Yanga bao tatu na la mwisho kwenye mchezo huo.

Kwa matokeo hayo, Yanga sasa inafikisha jumla ya pointi 15, katika michezo mitano waliocheza, huku wakiwa wameruhusu bao moja tu, kuingia nyavuni mwao.

Mara baada ya mchezo huo Ligi Tanzania Bara itasimama kupisha michezo ya kimataifa na kurejea tena tarehe 20 Novemba, 2021 ambapo Yanga itashuka dimbani dhidi ya Namungo FC.

error: Content is protected !!