Friday , 9 June 2023
Home Kitengo Michezo Yanga yaizaba Marumo, yaweka mguu mmoja fainali CAFCC
Michezo

Yanga yaizaba Marumo, yaweka mguu mmoja fainali CAFCC

Spread the love
  • WAWAKILISHI pekee katika Kombe la Shirikisho barani Afrika, Klabu ya Yanga SC imejiweka nafasi nzuri ya kutinga Fainali ya Michuano hiyo baada ya kuibuka na ushindi wa bao 2-0 dhidi ya Marumo Gallants ya nchini Afrika Kusini. Anaripoti Mwandishi Wetu …(endelea).

Ni katika mchezo wa mkondo wa kwanza wa  nusu fainali uliopigwa leo tarehe 10 Mei 2023 kwenye uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam.

Kipindi cha kwanza timu zote zilikuwa zikishambualiana kwa zamu na kwenda mapumziko zikiwa hazijafungana.

Kipindi cha pili timu zote zilifanya mabadiliko hata hivyo Yanga SC walinufaika na mabadiliko hayo mnamo dakika ya 64 baada ya Stephane Aziz Ki kuitanguliza Yanga Sc mbele kwa kufunga bao zuri akipokea pasi kutoka kwa Tusila Kisinda

Akitokea benchi kiungo mtukutu Benard Morrison alipigilia msumari wa pili katika dakika za jioni kabisa 90+2′ .

Timu hizo zinatarajia kurudiana katika mechi ya mkondo wa pili  tarehe 17 Mei 2023 nchini Afrika Kusini.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

HabariMichezo

Benki ya NBC yazindua kombe jipya la Ligi Kuu Tanzania Bara

Spread the loveMDHAMINI Mkuu wa Ligi ya NBC , Benki ya Taifa...

MichezoTangulizi

Yanga malizeni ugomvi na Fei Toto – Rais Samia

Spread the love  RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Samia...

Michezo

Samia aipongeza klabu ya Yanga kwa hatua iliyofikia

Spread the love RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Samia...

Michezo

Yanga waitwa Ikulu kesho Jumatatu

Spread the love RAIS wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, kesho Jumatatu, tarehe...

error: Content is protected !!