January 23, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Yanga yaitunishia misuli Bodi ya Ligi

Afisa Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano wa Yanga, Jerry Muro

Spread the love

KLABU ya Yanga imesisitiza itapeleka timu yake uwanjani kesho kwa ajili ya mechi dhidi ya Ruvu JKT na haitaenda uwanjani Machi 11 kama ilivyopangwa na Bodi ya Ligi.

Yanga imelalama kwamba Bodi ya Ligi imeahirisha mechi hiyo bila kukaa ikazungumza nao halafu ikaipeleka mbele hadi Machi 11 ikiwa ni siku tatu tu kabla ya kuivaa FC Platinum ya Zimbabwe.

Afisa wa Kitengo cha Mawasiliano wa Yanga, Jerry Muro amesema watapeleka timu uwanjani na kama mechi haitakuwepo, nao hawatapeleka timu Machi 11.

“Bodi ya ligi inapaswa kuwa wazi kuhusiana na mabadiliko, sisi tuko tayari kucheza kesho. Lakini si Machi 11.

“Angalia siku tatu mbele tuna mechi ya kimataifa, TFF inataka tucheze mechi ya ligi. Kwa nini tusicheze kesho halafu baada ya siku tatu tucheze na Simba.

“Baada ya hapo, tutapata nafasi ya maandalizi ya wiki moja kujiandaa na mechi ya kimataifa ambayo ni muhimu zaidi,” alisema Muro

error: Content is protected !!