January 25, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Yanga yaisambaratisha Mbeya City, Simba yachapwa na Stand

Mshambuliaji wa Yanga, Amisi Tambwe akishangilia bao lake alilofungwa akiwa sambamba na Simon Msuva

Spread the love

TIMU ya Yanga leo imeendelea ubabe wake katika jiji la Mbeya baada ya kuichakaza Mbeya City kwa mabao 3-1 katika mchezo uliochezewa kwenye Uwanja wa Kumbukumbu za Sokoine jijini Mbeya. Anaripoti Erasto Stanslaus … (endelea).

Kwa ushindi huo wa pili jijini Mbeya, Yanga imejikita kileleni baada ya kufikisha pointi 31 ambapo hata kama Azam FC wakishinda mchezo wao wa leo usiku dhidi ya Prisons hawatawaondoa kileleni.

Katika mechi hiyo iliyokuwa na mvutano kwa dakika zote 90, Yanga ndiyo walikuwa wa kwanza kupata bao la kuongoza lililofungwa na Simon Msuva dakika ya 18 kwa kichwa akiunganisha kazi nzuri iliyofanywa na kiungo Haruna Niyonzima. Hilo ni bao la tatu wa Msuva katika uwanja huo, baada ya kufunga mawili dhidi ya Prisons Alhamisi iliyopita walipoibuka na ushidni wa mabao 3-0.

Kipindi cha pili Mbeya City walianza kwa kasi kutaka kusawazisha bao hilo, lakini dakika ya 59 walijikuta wanaongezwa bao la pili na Mrisho Ngassa akitumia vizuri uzembe wa kipa wa timu hiyo, David Burhan aliyeshindwa kumiliki mpira aliorudishiwa na beki wake na kuporwa na mfungaji wa bao hilo.

Juhudi za Mbeya City zilizaa matunda dakika ya 69 baada ya Peter Mapunda kuipatia bao akiunganishwa kwa kichea krosi safi iliyochongwa na Steven Mazanda, lakini Amisi Tambwe alizima pilika za wapinzani wao dakika ya 78 alipoifungia Yanga bao la tatu kwa kichwa akiunganisha kona ya Niyonzima.

Katika mchezo mwingine uliochezwa kwenye Uwanja wa Kambarage mjini Shinyanga, timu ya Simba ilijikuta ikiangukia pua baada ya kushindwa kupata pointi wakiwa ugenini kwa kukubali kipigo cha bao 1-0 dhidi ya wenyeji wao Stand United.

Bao pekee lililofungwa na mchezaji wa kimataifa raia wa Nigeria, Abaslim Chidiabele dakika ya 11 ndiyo lililoizamisha Simba katika mchezo huo.

error: Content is protected !!