July 6, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Yanga yaipiga Simba mbele ya Rais Samia

Spread the love

 

TIMU ya Yanga ya Dar es Salaam, imeibuka na ushindi wa 1-0 dhidi ya watani zao Simba, katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara 2020/21. Anaripoti Kelvin Mwaipungu, Dar es Salaam … (endelea).

Mchezo huo umechezwa uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam, leo Jumamosi, tarehe 3 Julai 2021 na kushuhudiwa na maelfu ya mashabiki wa mpira akiwemo, Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan.

Goli pekee la Yanga, limefungwa dakika ya 11 ya kipindi cha kwanza kwa shuti kali la kiungo, Zawadi Mauya ambapo lilimgonga beki wa Simba, Shomari Kapombe na kuzama wavuni.

Ushindi huo, umewafanya Yanga kufikisha pointi 70 ikiwa na michezo miwili mkononi huku Simba ikisalia na pointi 73 na michezo minne.

Iwapo Simba ingeshinda, ingewafanya kutangazwa mabingwa wa ligi hiyo kwa msimu wa nne mfululizo.

error: Content is protected !!