January 28, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Yanga yaipiga Mgambo 2-0, yajikita kilele, Simba, Azam FC kesho

Washambuliaji wa Yanga, Simon Msuva na Amisi Tambwe waliofunga mabao mawili katika mchezo dhidi ya Mgambo wakishangilia mabao yao

Spread the love

TIMU ya Yanga leo imejikita kileleni mwa msimamo wa Ligi Kuu Tanzania Bara, baada ya kuitandika mbabe wa Simba, Mgambo Shooting mabao 2-0 katika mchezo uliochezwa kwenye Uwanja wa Mkwakwani, jijini Tanga. Anaripoti Erasto Stanslaus … (endelea).

Ushindi huo, unaifanya Yanga SC ifikishe pointi 37, baada ya kucheza mechi 18, ikiwazidi kwa pointi nne, Azam FC ambao hata hivyo wana mchezo mmoja mkononi wanacheza na Coastal Union kesho.

Katika mchezo huo ambao ulikuwa na ushindani mkubwa, Yanga walipata bao la kwanza dakika ya 77 ya mchezo huo, lililofungwa na Simon Msuva akiunganisha mpira wa kichwa wa Kper Sherman akiunganisha krosi ya Haruna Niyonzima.

Bao hilo liliahamsha hasira za Mgambo na kucheza kwa kushambulia ili kupata bao la kusawazisha, lakini walijikuta wakifungwa bao la pili dakika ya 83, mfungaji akiwa Amisi Tambwe akimalizia krosi ya Msuva.

Simba ambao walikubali kipigo cha mabao 2-0 na Mgambo katika mchezo wao uliopita uliochezwa Jumatano iliyopita jijini Tanga, watashuka dimbani kesho kuvaana na Ruvu Shooting katika Uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam.

error: Content is protected !!