January 17, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Yanga yaipiga Mbeya Kwanza, yaisubiri Simba

Spread the love

 

TIMU ya Yanga imeendelea kujichimbia kileleni mwa Ligi Kuu ya Tanzania Bara 2021/22, kwa kuibuka na ushindi wa 2-0 dhidi ya Mbeya Kwanza. Anaripoti Mwandishi Wetu…(endelea).

Yanga imeibuka na ushindi huo leo Jumanne, tarehe 30 Novemba 2021, katika Uwanja wa Sokoine, jiji Mbeya. Magoli hayo yamefungwa na Saido Ntibazonkiza kwa shuti la faulo nje ya 18 na jingine likifungwa na Fiston Mayele akiunganisha pasi safi ya Feisal Salim ‘Fei Toto.’

Ushindi huo, umewafanya kuendelea kusalia kilele ikifikisha pointi 19 kati ya michezo saba nyuma ya watani zao Simba, yenye pointi 14 baada ya kushika dimbani mara sita na kesho Jumatano, Simba itacheza na Geita, Uwanja wa Mkapa, Dar es Salaam.

Mchezo unaofuata ni wa Yanga kuumana na watani zao Simba, kuanzia saa 11:00 jioni ya tarehe 11 Desemba 2021, katika Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam.

Yanga itashuka dimbani ikiwa na kumbukumbu nzuri ya kuwapiga watani zao 1-0, katika mchezo wa Ngao ya Jamii.

error: Content is protected !!