May 26, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Yanga yaipiga Gwambina, yazidi kuikimbia Simba

Spread the love

 

MABINGWA wa kihistoria Tanzania Bara, Yanga ya Dar es Salaam, imeendeleza vipigo kwenye ligi kuu nchini humo, kwa kuifunga 3-1, Gwambina FC ya mkoani Mwanza. Anaripoti Kelvin Mwaipungu, Dar es Salaam … (endelea).

Yanga imeibuka na ushindi huo wa pili mfululizo leo Jumanne, tarehe 20 Aprili 2021, katika Uwanja wa Benjamin Mkapa, mkoani Dar es Salaam na kuwafanya kufikisha pointi 57 kati ya michezo 26.

Siku tatu zilizopita, Yanga iliibuka na ushindi wa 1-0 dhidi ya Biashara United katika uwanja huo huo.

Magoli hayo ya Yanga, yamefungwa na mshambuliaji aliyekuwa na ukame wa magoli kwa zaidi yam waka mmoja, Ditram Nchimbi, dakika ya 18, kwa shuti kali, alilolipiga nje ya 18 na kwenda moja kwa moja langoni.

Timu hizo, zilikwenda mapumziko huku Yanga ikiwa mbele kwa goli moja. Gwambina iliwachukua dakika nne, kusawazisha kupitia kwa Jimson Mwanuke dakika ya 49 kwa shuti kali, lililomshinda mlinda mlango wa Yanga, Farouk Shikalo.

Shangwe hizo za Gwambina, hazikudumu kwani dakika mbili kwani dakika ya 52, mlinzi wa Yanga, Bakari Mwamnyeto aliifungia goli la pili kwa picha akiunganisha kona iliyopigwa na Carlos Carlinhos.

Yanga walipata bao la tatu dakika ya 90+4, lililofungwa na Saidi Ntibazonkiza baada ya kuwachambua mabeki wa Gwambina na kumchambua kipa na kukwamisha mpira wavuni.

Wakati Yanga ikiendelea kujiweka kileleni, watani zao Simba itakuwa ugenini kesho Jumatano kucheza na Kagera Sugar, katika Uwanja wa Kaitaba mkoani Kagera.

Yanga

Simba itashuka ndimbani ikiwa na pointi 52 ikiwa imecheza michezo 22 huku Yanga yenyewe ikicheza michezo 26, tofauti ya michezo minne.

Mechi hiyo ya Yanga, imeshuhudiwa na kocha wake mpya, Mohamed Nasreddine Al- Nabi, raia wa Misri, akiwa jukwaani.

Nabi ametambulishwa leo mchana Jumanne, baada ya kuingia mkataba wa miezi 18 kuwafundisha Yanga wanaowania ubingwa wa ligi kuu, ambao wameukosa kwa miaka mitatu mfululizo.

Anachukua nafasi ya Cerdic Kaze, raia wa Burundi, aliyefukuzwa Machi 2021. Naye Nadi anajiunga na Yanga baada ya kufukuzwa na timu ya El Merrikh ya Sudan aliyoifundisha kwa siku takribani 40.

error: Content is protected !!