January 23, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Yanga yaibonyeza tena Simba, warudi kileleni

Spread the love

HESHIMA imerudi mahali pake, baada ya Yanga kuituliza tena Simba kwa kipigo cha mabao 2-0 katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara, uliochezwa kwenye Uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam, anaandika Erasto Masalu.

Mabao ya Donald Ngoma na Amissi Tambwe yalitosha kuwarudisha Yanga kileleni katika msimamo wa Ligi Kuu Tanzania Bara baada ya kufikisha pointi 46 huku wakiiporomosha Simba iliyokuwa kileleni mpaka nafasi ya tatu wakiwa na pointi 45. Azam wanashika nafasi ya pili.

Mchezo huo ambao ulianza kwa ushindani mkubwa, lakini Simba walipata pigo dakika ya 26 baada ya beki wake wa kati, Abdul Banda kutolewa kwa kadi nyekundu baada ya kupewa kadi mbili za njano.

Yanga walitumia vizuri makosa wa beki wa kulia wa Simba, Hassan Kessy aliyerudisha mpoira mfupi kwa kipa wake, Vicent Angban kabla ya kudakwa na Ngoma na kumpiga chenga kipa na kukwamisha mpira wavuni.

Bao la pili la Yanga lilifungwa na Tambwe aliyetumia juhudi za ziada kuunganisha krosi ya Geofrey Mwashiuya iliyomshinda kipa wa Simba na kuandika bao lililodumu mpaka dakika ya mwisho ya mchezo huo.

Matokeo mengine ya michezo ya leo ya Ligi Kuu Bara haya hapa chini.

Toto 1 Kagera 1

Mgambo 1 Prisons 1

Stand 1 JKTRuvu 1

Mbeya City 0 Azam 3

error: Content is protected !!