January 28, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Yanga yaibeba Ndanda, Polisi, Ruvu bye bye

Wachezaji wa Yanga na Ndanda wakipambana katika mchezo wa kwanza uliochezwa Uwanja wa Taifa.

Spread the love

USHINDI wa bao 1-0 walioupata timu ya Ndanda FC dhidi ya Yanga imeisaidia timu hiyo kubaki katika Ligi Kuu Tanzania msimu ujao. Anaandika Erasto Stanslaus … (endelea).

Ndanda ambayo moja kati ya timu zilizokuwa zinahatihati ya kushuka daraja kutokana na kuwa na pointi 28, lakini ushindi walioupata kwenye Uwanja wa Nangwanda mjini Mtwara wamefikisha pointi 31 hivyo kuwa salama kubaki ligi hiyo mwakani.

Timu ambazo zimekumbwa na wimbi la kushuka daraja ni Polisi Morogoro, Mgambo Shooting na Ruvu Shooting ambazo pointi zao hazijatosha kubaki msimu ujao na nafasi zao zinachukuliwa na Mwadui FC ya Shinyanga, Toto Africans ya Mwanza, Majimaji ya Ruvuma na Africans Sports ya Tanga.

Polisi ambayo leo imekubali kichapo cha bao 1-0 kutoka kwa Mbeya City, imemaliza msimu huu ikiwa kileleni baada ya kucheza michezo 26 na kuvuna pointi 25.

Mgambo Shooting imefanikiwa kubaki Ligi Kuu baada ya kuikaba koo Azam FC kwenye Uwanja wake wa nyumbani wa Chamazi kwa kuilazimisha suluhu, hivyo kumaliza ikiwa nafasi ya 12 ikiwa na pointi 29.

Ruvu Shooting nayo inarudi ligi daraja la kwanza baada ya kukubali kichapo cha bao 1-0 na Stand Ubited mchezo uliochezwa kwenye uwanja wa Kambarage  mjini Shinyanga na kuifanya imalize nafasi ya 13 ikiwa na pointi 29.

[pullquote]

MATOKEO YA LEO

JKT Ruvu 1-2 Simba
Azam FC 0-0 Mgambo
Stand United 1-0 Ruvu 
Mbeya City 1-0 Polisi
Ndanda 1-0 Yanga
Kagera 0-0 Prisons
Mtibwa 1-2 Coastal Union

[/pullquote]

Yanga wametwaa ubingwa huo wakiwa na pointi 55, huku nafasi ya pili ikichukuliwa na Azam FC yenye pointi 49, nafasi ya tatu imeenda kwa Simba iliyovuna pointi 47, wakati nafasi ya nne imeenda kwa Mbeya iliyofikisha pointi 34.

Timu ya Coastal Union imeshika nafasi ya tano ikiwa na pointi 34, nafasi ya sita imekaliwa na Kagera Sugar wenye pointi 32, Mtibwa Sugar wamemaliza nafasi ya saba wakiwa na pointi 31, Ndanda FC wamemaliza nafasi ya nane wakiwa na pointi 31, wakifuatiwa na Stand United wenye pointi 31.

Nafasi ya 10 imechukuliwa na JKT Ruvu wenye pointi 31 wakati timu ya Prisons imeponea chupuchupu kushuka daraja baada ya kumaliza ikiwa na nafasi ya 11 ikiwa na pointi 29.

error: Content is protected !!