July 1, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Yanga yaibania Simba kupanda ndege

Warembo wa Vodacom wakiwa na Kombe la Ubingwa na medali, tayari kwa kuwakabidhi Yanga

Spread the love

KLABU ya Simba italazimika kusubiri kwa msimu mwingine kukata tiketi ya kucheza michuano ya kimataifa, baada ya Yanga kukubali kichapo cha mabao 2-1 katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara uliochezwa leo. Anaandika Erasto Stanslaus … (endelea).

Kwa matokeo hayo Azam FC imekata tiketi ya kucheza Kombe la Shirikisho Afrika mwakani, baada ya kufikisha pointi 48 baada ya kucheza mechi 25, nyuma ya mabingwa, Yanga SC wenye pointi 55 za mechi 25.

Simba SC ipo nafasi ya tatu kwa pointi zake 44 na hata ikishinda mechi yake ya mwisho itafikisha 47, hivyo kwa mwaka wa tatu mfululizo Wekundu wa Msimbazi watakosa michuano ya Afrika.

Azam FC ilitoka nyuma kwa 1-0 baada ya Mbrazil Andrey Coutinho kutangulia kuifungia Yanga SC dakika ya 12 na Bryson Raphael akasawazisha dakika ya 14 kabla ya Aggrey Morris kufunga la ushindi dakika ya 85.

Baada ya mchezo huo kumalizika timu ya Yanga walikabidhiwa kombe lao la Ubingwa la msimu wa 2014/15 na kufanya kuweka kabatini makombe 25 ya Ligi Kuu Tanzania Bara.

error: Content is protected !!