May 29, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Yanga yaibamiza Mwadui FC, yatinga nusu fainali FA

Spread the love

 

Ushindi wa mabao 2-0, dhidi ya Mwadui FC kwenye robo fainali ya pili ya michuano ya kombe la Shirikisho (Azam Federation Cup) umeifanya klabu ya Yanga kutinga hatua ya nusu fainali ya michuano hiyo ambapo wataminyana na Biashara United. Anaripoti Kelvin Mwaipungu…(endelea)

Mchezo huo ulichezwa kwenye Uwanja wa CCM Kambarage Shinyanga na Mwadui ambao wameshuka daraja kwenye Ligi Kuu waliaga rasmi michuano hiyo kwenye msimu huu.

Iliwachukua Yanga dakika 22 kwa Yanga kuandika bao la kwanza kupitia kwa Deus kaseke mara baada ya mlinda mlango wa Mwadui Fc kufanya makossa na kunyang’anywa mpira na kuwekwa kambani.

Mchezo huo uliendelea ambapo Yanga walitengeneza nafasi nyingi za mabao na kushindwa kuzitumia na kufanya mchezo huo kwenda mapumziko Yanga wakiwa mbele kwa bao 1-0.

Kipindi cha pili kilirejea na Yanga kuonekana kulisakama lango la Mwadui na kwenye dakika ya 56, Deus Kaseke tena lipachika bao la pili mara baada ya kupokea pasi ya kichwa kutoka kwa Yacouba Songne na matokeo hayo kudumu mpaka dakika 90 zilipokamilika.

Kwa matokeo hayo Yanga itakutana na Biashara United ambayo iliwaondosha Namungo FC, mchezo utakaopigwa kwenye dimba la Al Hassan Mwinyi mkoani Tabota tarehe 12 Juni 2021.

Yanga waliingia kwenye mchezo huo huku ikikosa huduma za wachezaji wake nane ambao walikuwa nje ya Uwanja kwa sababu tofauti tofauti.

Yassin Abdallah, Carlos Carlinhos, Abdallah Shaibu pamoja na Saido Ntibanzokiza wao walikosa mchezo huo mara baada ya kusumbuliwa na majeruhui huku kwa upande wa Lamine Moro, Metacha Mnata na Michael Sarpong wameondolewa kwenye kikosi hiko kutokana na utovu wa nidhamu, huku Haruna Niyonzia akiwa nje kwa matatizo ya kifamilia.

Nusu Fainali ya tatu na nne ya michuano hiyo itaendelea hii leo ambapo Azam FC itakuwa ugenini mkoani Tabora kuminyana na Rynho Rangers, huku Mabingwa watetezi wa michuano hiyo klabu ya Simba itashuka kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa majira ya saa 1 usiku kuwakalibisha Dodoma Jiji FC.

Ikumbukwe Fainali ya michuano hiyo kwa mwaka huu itapigwa mkoani Kigoma.

error: Content is protected !!