May 27, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Yanga yafunga usajili na ushindi

Spread the love

CHIKO Ushindi aliyekuwa winga wa klabu ya TP Mazembe ya nchini Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo amekamilisha usajIli wa kujiunga na klabu ya Yanga kwa mkataba wa mwaka mmoja. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea)

Mchezaji huyo ametambulishwa leo tarehe 16 Januari 2022 na klabu hiyo muda mchache kabla ya kuanza mchezo wao wa Ligi Kuu Tanzania Bara dhidi ya Coastal Union ambao Yanga waliibuka na ushindi wa mabao 2-0.

Ushindi amesajiliwa ikiwa dakika za mwisho kabla ya kufungwa kwa dirisha dogo la usajili la mwezi Januari, ambalo lilidumu kwa kipindi cha mwezi mmoja.

Yanga wanafanya usajili huo na kutimiza idadi ya wachezaji 11 wa kigeni kati ya 12 wanaoruhusiwa kikanuni Katika mashindano ya Ligi Kuu Tanzania Bara kwa msimu huu wa 2021/22.

Usajili huu unafanya Yanga kusajili jumla ya wachezaji watano kwenye dirisha dogo la usajili toka lilipofunguliwa Desemba 16, 2021 na kufungwa Januari 15 majira ya saa 6 kamili usiku.

Wachezaji ambao mpaka sasa wamesajiliwa na Yanga ni Salum Abubakar, Crispin Ngushi, Denis Nkane na Aboutwalib Mshery ambaye ni mlinda mlango akitokea klabu ya Mtibwa Sugar.

Aidha klabu hiyo hakuishia kwenye usajili wa Chiko Ushindi tu, aidha siku ya leo ilifanikiwa tena kutangaza usajili wa kocha wa magolikipa Milton Nievon ambaye alikuwa akiwanoa walinda mlango wa klabu ya Simba.

Usajili wa Milton ndani ya klabu ya Yanga huenda ukamuondoa kocha wa makipa wa sasa wa klabu hiyo Razak Siwa ambaye ni raia wa Kenya.

Niovan aliondoka kwenye klabu ya Simba mara baada ya uamuzi wa bodi ya timu hiyo kufanya mabadiliko kwenye benchi la ufundi kwa kumfungashia virago aliyekuwa kocha mkuu wa klabu hiyo Didie Dalosa pamoja na baadhi ya wafanyakazi kwenye benchi lake kufuatia timu hiyo kupata matokeo mabovu kwenye michuano ya Ligi ya mabingwa Afrika.

error: Content is protected !!