Sunday , 29 January 2023
Home Kitengo Michezo Yanga yafunga mwaka kwa kishindo
Michezo

Yanga yafunga mwaka kwa kishindo

Spread the love

 

KLABU ya soka ya Yanga imefanikiwa kufunga mwaka 2021 kwa kishindo mara baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 4-0, dhidi ya Dodoma Jiji FC kwenye Ligi Kuu Tanzania Bara. Anaripoti Kelvin Mwaipungu…(endelea)

Mchezo huo ulipigwa hii leo tarehe 31 Desemba, 2021 kwenye dimba la Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam majira ya saa 1 usiku.

Kwenye mchezo huo ambao Yanga walitawala mpira kwa asilimia kubwa walifanikiwa kuandika bao lao la kwanza kupitia kwa Fiston Mayele kwenye dakika ya 42, na kufanya bao hilo kudumu hadi mapumziko.

Kipindi cha pili kiliporejea Yanga ilionekana kuimalika zaidi ya Dodoma Jiji na kufanikiwa kuandika bao la pili kwenye dakika ya 56 kupitia kwa Jesus Moloko mara baada ya kuunganisha mpira mrefu uliopigwa na mlinzi wao wa kati Yanick Bangala.

Mara baada ya kupata bao hilo Yanga haikuishia hapo, iliendelea kupeleka mashambulizi kwenye lango kiasi cha kupelekea mlizni wa Dodoma Jiji Justine kujifunga bao kwenye dakika ya 71 baada ya kuugusa mpira uliopigwa na Feisal Salum.

Kalamu ya mabao kwa upande wa Yanga kwenye mchezo huo ilitamatishwa na Khalid Aucho ambaye alimpigilia msumari wa bao la nne dakika ya 81.

Kwa matokeo hayo Yanga inaendelea kujikita kileleni ikiwa na alama 29, huku nafasi ya pili ikishikwa na Simba wenye alama 21 baada ya kucheza michezo tisa.

Ligi kuu hiyo itaendelea kesho kwa kupigwa mchezo kati ya Simba ambao watawalika Azam Fc kwenye dimba la Benjamin Mkapa majira ya saa 1 usiku.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Michezo

GGML: Uwanja mpya wa Geita Gold FC kukamilika Mei, 2023

Spread the loveUWANJA wa Magogo unaojengwa na Halmashauri ya Mji wa Geita...

Michezo

Wanafunzi chuo Mwalimu Nyerere wapongezwa kwa ushindi

Spread the love  UONGOZI wa Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere (MNMA)...

Michezo

Arsenal waipopoa Manchester United

Spread the loveKLABU ya Arsenal inayoshiriki Ligi Kuu England imewatandika Mashetani Wekundu...

Michezo

Mchezaji Singida apoteza maisha mazoezini

Spread the love  MCHEZAJI na kapteni wa timu ya vijana ya Singida...

error: Content is protected !!