January 23, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Yanga yafanya kufuru Taifa, Azam yabanwa kwao

Washambuliaji wa Yanga, Simon Msuva na Amissi Tambwe wakishangilia moja ya mabao yao

Spread the love

HII ni sifa sasa. Hayo ndiyo maneno unayoweza kusema kwa matokeo yaliyotokea kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam katika mechi kati ya Yanga na Coastal Union ambayo imemalizika kwa Wagosi wa Kaya kukubali kichapo cha mabao 8-0.

Katika mchezo huo wa Ligi Kuu Bara, Yanga ilionyesha imepania ushindi baada ya kwenda mapumziko ikiwa inaongoza kwa mabao matatu.

Kipindi cha pili kilikuwa na mabao mengine matano na Amissi Tambwe alifanikiwa kufunga mabao manne, Simon Msuva mawili, Salum Telela na Kper Sherman akaona mwezi kwa kucheka na nyavu

Yanga imezidi kujichimbia kileleni baada ya kufikisha pointi 43.

Azam FC yenye inabaki katika nafasi ya pili baada ya sare ya bao 1-1 dhidi ya Mbeya City kwenye Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Dar.

Sare hiyo imeifanya Azam FC kufikisha pointi 37 lakini ina  mchezo mmoja pungufu kwa Yanga.

error: Content is protected !!