May 20, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Yanga yabanwa mbavu na KMC

Spread the love

 

TIMU  ya KMC imewabana mbavu Yanga kwa kuwalazikisha  sare ya bao 1-1, katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara uliopigwa kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam. Anaripoti Kelvin Mwaipungu, Dar es Salaam … (endelea). 

Mchezo huo wa kwanza kwa Yanga toka kurejea kwa Ligi Kuu baada ya kusimama kwa wiki tatu kupisha michezo ya kimataifa pamoja na maombelezo kufuatia kifo cha aliyekuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Hayati John Magufuli.

Kwenye mchezo huo KMC walikuwa wa kwanza kupata bao kupitia kwa Braison David dakika ya 33 na kufanya mchezo huo kwenda mapumziko Yanga ikiwa nyuma kwa bao 1-0.

Kipindi cha pili kilirejea na Yanga walifanikiwa kusawazisha bao hilo kupitia kwa Yacouba Sogne dakika ya 46 kwa kichwa.

Mara baada ya kusawazisha bao hilo timu hizo mbili zilionekana kushambuliana kwa kasi lakini hakuna timu iliofanikiwa kuona tena lango la mwenzake

Kwa matokeo hayo Yanga itaendelea kusalia kileleni ikiwa na pointi 51, baada ya kucheza michezo 24. Simba inashika nafasi ya pili ikiwa na pointi 46 wakiwa wamecheza michezo 23.

error: Content is protected !!