May 20, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Yanga yabanwa mbavu na Kagera Sugar

Spread the love

 

KLABU ya Yanga imelazimishwa sare ya mabao 3-3 na Kagera Sugar kwenye mchezo wa Ligi Kuu Soka Tanzania Bara. Anaripoti Kelvin Mwaipungu, Dar es Salaam … (endelea).

Mchezo huo wa mzunguko wa 20 wa Ligi Kuu ulichezwa kwenye Uwanja wa Mkapa jijini Dar es Salaam majira ya saa 1 usiku.

Kagera Sugar walikuwa wa kwanza kupata bao kupitia kwa Peter Mwalianzi dakika ya 11, na baadae Yanga walifanikiwa kusawazisha kwa njia ya mkwaju wa penati iliyopigwa na Tuisila Kisinda dakika ya 14.

Kagera Sugar walifanikiwa kurudi mchezoni na kuandika bao la pili dakika 26, na Deus Kaseke akaisawazishia Yanga na dakika 30, baadae Yusuph Muhilu aliandika bao la tatu na kufanya mchezo huo kwenda mapumziko kwa matokeo ya 3-2.

Kipindi cha pili kilianza kwa kocha wa Yanga Cedric Kaze kufanya mabadiliko kwa kumtoa Zawadi Mauya na nafasi yake kuchukuliwa na Mukoko Tonombe ambaye aliifungia timu yake bao la tatu dakika ya 61.

Kwa matokeo hayo Yanga inaendelea kuwa kileleni wakiwa na pointi 46, baada ya kucheza michezo 20, huku Simba ikiwa kwenye nafasi ya pili ikiwa na pointi 49 na michezo 17.

error: Content is protected !!