September 23, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Yanga yaanza kimataifa kwa kipigo

Spread the love

 

MABINGWA wa kihistoria wa soka nchini Tanzania, Yanga ya jijini Dar es Salaam wameanza vibaya safari ya michuano ya klabu bingwa Afrika kwa kukubali kipigo cha 1-0 kutoka kwa Rivers United ya Nigeria. Anaripoti Kelvin Mwaipungu, Dar es Salaam … (endelea).

Yanga imeanza safari yake kwenye michuano hiyo leo Jumapili, tarehe 12 Septemba 2021, katika dimba la Benjamin Mkapa, mkoani Dar es Salaam.

Ili Yanga walioingia dimbani wakiwa na kauli mbiu ya ‘Return of the Championi’ wasonge hatua inayofuata, watalazimika kushinda mchezo wa marudiano, wiki mbili zijazo nchini Nigeria.

Goli pekee lililopeleka kilio kwa vijana hao wa Jangwani, limefungwa dakika ya 51 na Omoduemuke Moses kwa kichwa baada ya mabeki wa Yanga, kujichanganya.

Kutokana na ugonjwa wa corona, mchezo huo umechezwa bila mashabiki.

error: Content is protected !!