Saturday , 13 April 2024
Home Kitengo Michezo Yanga wazidi kupukutika
Michezo

Yanga wazidi kupukutika

Spread the love

MAKAMU Mwenyekiti wa Yanga, Clement Sanga ametangaza kujiuzulu nafasi yake ya uongozi ndani ya klabu hiyo kutokana na kusambaa kwa kipande cha video kikionesha wanachama wa klabu hiyo kuhamasishana kwenda kumfanyia fujo nyumbani kwake na mapanga. Anaripoti kelvin Mwaipungu … (endelea).

Video hiyo ambayo ilikuwa ikimuonesha mwanachama maarufu wa klabu anayefahamika kwa jina la JITU kutoka tawi la Tandale akimtaka kiongozi huyo kujiuzulu mwenyewe kwa hiari yake, la sivyo wanachama watakwenda kumfanyia fujo nyumbani kwake.

“Nimejiuzulu rasmi nafasi yangu ya Makamu Mwemyekiti wa klabu ya Yanga, baada ya mashabiki kuhamasishana kuja nyumbani kwangu na mapanga kuja kunidhuru, najua maamuzi yangu yatawaumiza baadhi ya wanayanga kwa kuwa mimi nina familia na nisingependa kuendelea katika hali hii,” amesema Sanga.

Sanga anakuwa kiongozi wa pili kujiuzulu ndani ya klabu ya Yanga katika kipindi cha saa 48, baada ya katibu mkuu wa klabu hiyo Mkwasa kufanya hivyo siku ya jana kutokana na kusumbuliwa na maradhi.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Michezo

Usiku wa Ulaya kinawak tena leo

Spread the love  LIGI ya mabingwa barani ulaya itaendelea tena leo ambapo...

Michezo

Ligi ya Mabingwa Barani Ulaya ni Usiku wa Kisasi

Spread the love  LEO utarejea ule usiku pendwa kabisa kwa mashabiki wa...

BurudikaMichezo

Kizz Daniel aunguruma na EP mpya ‘Thankz alot’

Spread the loveMKALI wa muziki nchini Nigeria, Kizz Daniel ametoa EP yake...

MichezoTangulizi

Samia aipa tano Yanga

Spread the loveRAIS Samia Suluhu Hassan ameipongeza Klabu ya Yanga licha ya...

error: Content is protected !!