MARA baada ya kuangukia kwenye michuano ya kombe la Shirikisho, klabu ya soka ya Yanga imepangwa kumenyana dhidi ya Club Africain ya nchini Tunisia, katika mchezo wa mtoano. Anaripoti Damas Ndelema…(endeleaa)
Droo ya michezo hiyo imechezeshwa hii leo tarehe 18 2022, jijini Cairo nchini Misri ambapo ndio makao makuu ya Shirikisho la Mpira Barani Afrika (CAF)
Katika mchezo huo Yanga itaanzia nyumbani kwenye dimba la Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam, tarehe 2 Novemba 2022, kwenye dimba la Benjamini Mkapa jijini Dar es Salaam, huku mchezo wa marudiano ukitarajia kupigwa nchini Tunisia tarehe 9 Novemba 2022.
Yanga imeangukia kwenye michuano hiyo, mara baada ya kuondolewa na Al Hilal ya nchini Sudan, kwa jumla ya mabao 2-1 katika michezo yote miwili.
Kwa upande wa Club Africain wao walifanikiwa kufuzu kwa hatua hii, mara baada ya kuwaondosha Kipanga ya Zanzibar kwa jumla ya mabao 7-0, katika mchezo wa marudiano huku mchezo wa kwanza uliopigwa Zanzibar Oktoba 8 mwaka huu, walitoka sare ya bila kufungana.
Mapendekezo yetu ni kuona Yanga ikishinda ila ni vigumu saana tena saana Yanga kuwashinda CLUB AFRICAIN. Club hii ni bora zaidi mara ine kuliko hata Al hilal ambayo iliwatowa Yanga week iliopita. Ila soccer ni soccer labda club yetu ya Yanga inaweza kupata nafasi kushinda michuwano yao