January 28, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Yanga wamvaa Mwenyekiti Simba

Spread the love

Uongozi wa Klabu ya Yanga umeeleza kusikitishwa na kauli iliyotolewa na Mwenyekiti wa Klabu ya Simba, Murtaza Mangungu kutokana na tuhuma alizoishusha Yanga baada ya mchezo nambari 64 wa Ligi Kuu baina ya Simba SC na Yanga uliochezwa jana tarehe 11 Disemba mwaka huu. Anaripoti Mwandishi Wetu… (endelea)

Hatua hiyo imekuja baada ya Mangungu kuishutumu klabu ya Yanga kuwa kuna watu wao waliingia katika eneo la VVIP ndani ya uwanja wa Mkapa jijini Dar es Salaam bila kuwa na kadi.

Hayo yametokea ilihali Mtendaji Mkuu wa Simba, Barbara Gozalez akizuiwa kuingia katika eneo hilo.

Pia Mangungu aliituhumu Shirikisho la Soka nchini –TFF kwamba ina dhumuni la kuipa ubingwa Yanga msimu huu wa mwaka 2021/2022.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Yanga leo tarehe 12 Disemba, 2021 imesema kauli hizo za Mangungu si za kiungwana na zimechafua taswira ya Klabu hiyo na kuleta sintofahamu kubwa kwa wanachama wao, wanamichezo, wadhamini na wadau mbalimbali.

“Klabu yetu haihusiki kabisa na utaratibu wa kuingia uwanjani kwa wageni wa VVIP, hivyo tumeshangazwa na shutuma zilizotolewa na Mangungu.

“Sisi kama wageni wa mchezo tulipatiwa kadi 30, VVIP zikiwamo 20 na VIP 10. Hivyo kauli kuwa watu wa Yanga wameonekana wamepita bila kuwa na tiketi au kadi ni kutaka kuonesha kuwa Kalbu ya Yanga haifuati utaratibu na inapata upendeleo kutoka TFF kitu ambacho siyo ksahihi na kinapelekea ujumbe mbaya kwa jamii yetu.

error: Content is protected !!