Saturday , 20 April 2024
Home Gazeti Habari Yanga waiweka Simba mtegoni
HabariMichezo

Yanga waiweka Simba mtegoni

Spread the love
WAKATI ligi Kuu Tanzania Bara ikiwa ukingoni, huku bado kukiwa na vita ya ubingwa Kati ya mafahari wawili wa soka la Tanzania, kkabu ya Yanga ambao ndio vinara wa Ligi hiyo mpaka Sasa wameweka Simba kwenye mtego mkubwa kuelekea mchezo wao dhidi ya Azam Fc. Anaripoti Mwandishi Wetu…(endelea)
Mchezo huo wa mzunguko wa 24, utapigwa kesho majira ya saa 1 usiku kwenye dimba la Azam Complex Chamazi ambapo Azam Fc ndio atakuwa mwenyeji wa mchezo huo.
Mpaka Sasa kuelekea kwenye mafanikio ya ubingwa kwa msimu huu, Yanga kwa sasa anahitaji alama 11, Sawa na kushinda michezo minne Kati ya Sita iliyobaki kukamilisha duru la pili.
Huwenda michezo hiyo minne ambayo Yanga anahitaji kushinda isifike kutokana na kutegemea matokeo ya Simba katika michezo yake hiyo saba iliyobaki.
Mpaka Sasa Yanga yupo kileleni akiwa na pointi 60, alama 11 nyuma ya Simba waliokuwa kwenye nafasi ya pili wakiwa na pointi zao 11 na michezo 23 na endapo kama walishinda michezo Yao yote iliyosalia watafikisha Jumla ya alama 70.
Kwa sasa viongozi wengi wa kkabu ya Yanga hata benchi la Ufundi, you wamenukuliwa Mara kadhaa wakisema bado wanakazi ya kufanya katika kuzisaka hizo pointi 11 licha ya kupewa nafasi kubwa ya kutwaa ubingwa kwa Mara 28 katika historia ya Ligi Kuu.
Pamoja na hayo lakini kwa sasa, Yanga kwa sasa kama wameweka Simba mtegoni kwenye michezo Yao miwili inayokuja mbele, huku wakiamini wanaweza kudondosha alama na kufanya idadi ya michezo wanayohitaji kushinda kupungua, kutokana na aina ya Timu wanaoenda kucheza nazo na rekodi waliokuwa nayo kwa michezo ya ugenini kwa msimu huu.
Simba kesho inaminyana na Azam FC ugenini, huku wakiwa hawana rekodi ya kupata matokeo kwenye dimba hilo la Azam Complex, katika michezo yote miwili waliyocheza na Azam F  ambayo ilimalizika kwa sare.
Mtego mwengine ambao Yanga wanaamini Simba anaweza kudondosha alama ni mchezo ujao Mara baada ya kucheza na Azam FC, ambapo itawalazimu kusafiri mpaka mkoani Geita kumenyana na moja ya timu ngumu kwa msimu huu Geita Gold FC.
Geita imekuwa ni timu ambayo imepata matokeo Mazuri wakiwa kwenye dimba lao la nyumbani, ambapo mpaka wamepoteza mchezo mmoja tu nyumbani dhidi ya Yanga kwa bao la mapema lilowekwa Kambani na Fiston Kalala Mayele.
Hayo yote yanashabihishwa na aina ya matokeo ambayo amekuwa akiyapata Simba kwenye viwanja vya mikoani toka kuanza kwa msimu huu wa mashindano wa 2021/21.
Alama nyingi kwa msimu huu, and Simba amezidondosha katika viwanja vya mikoani kwa kutoa sare nne dhidi ya Mtibwa Sugar, Polisi Tanzania, Namungo Fc na Biashara United huku akipoteza kwenye michezo dhidi ya Mbeya City na Kagera Sugar.
Kama Simba itafanikiwa kupata ushindi katika michezo hiyo miwili migumu ijayo basi itawalazimu Yanga kushinda michezo hiyo minne inayohitajika ili kutwaa taji Hilo ambalo wamelikosa katika kipindi cha miaka minne likiwa chini ya utawala wa Simba ambao walionekana kufanya vizuri.
Kwa mujibu wa kalenda ya bodi ya Ligi ambacho ni chombo Kinachosimamia Ligi hiyo, Inaonesha kuwa Ligi hiyo itamalizika mwishoni mwa mwezi wa Sita.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Michezo

Tusua mkwanja na mechi za Ijumaa leo

Spread the love  LEO hii mechi zinaendelea kote na wewe kama unataka...

Michezo

Piga pesa na mechi za EUROPA leo hii

Spread the love Hatimaye Alhamisi ya EUROPA imefika ambapo leo hii mechi...

Michezo

Leo ni leo nani kutinga nusu fainali UEFA?

Spread the love HATIMAYE Jumanne ya UEFA imefika ambapo leo hii michezo...

Michezo

Anza Jumatatu yako na Meridianbet

Spread the love  IKIWA ni siku nyingine mpya kabisa ya Jumatatu baadhi...

error: Content is protected !!