Katika michuano hiyo, iliyohitishwa jana jijini Algers, Algeria, Yanga waliondolewa kwa kanuni ya bao la ugenini, kufuatia ushindi wake wa bao moja kwa sifuri, kufuatia kuruhusu mabao mawili kwa moja katika mchezo wake wa kwanza jijini Dar es Salaam, wiki iliyopita.
Yanga ambayo ni mabingwa kwa mara ya pili mfululizo wa Ligi Kuu ya NBC, ilikutana na USM Alger ya Algeria, 28 Mei katika uwanja wa Mkapa jijini Dar es Salaam, ambapo vijana hao wa Jangwani waliruhusu mabao hayo mawili.
Mhe. Rais Dkt. @SuluhuSamia awaalika Wananchi @yangasc1935 kula nae chakula cha jioni Ikulu, Dar es Salaam kesho Juni 05, 2023.
Asante Mhe. Rais
Heshima kubwa kwa Wananchi @yangasc1935 pic.twitter.com/5T0KlqwT8f— Gerson Msigwa (@MsigwaGerson) June 4, 2023
Taarifa iliyotolewa na Msemaji wa Serikali, Gerson Msigwa, imeeleza kuwa Rais Samia amewapongeza Yanga kwa kucheza vizuri katika mchezo wa pili wa fainali hapo jana kwa kuwafunga wenyeji wa mchezo huo bao 1-0 na hivyo kuwa na matokeo ya jumla ya mabao 2-2 japokuwa hawakufanikiwa kutwaa ubingwa wa kombe hilo.
Amesema, pamoja na kutotwaa ubingwa, Rais Samia anatambua kuwa Yanga wameipa heshima kubwa Tanzania na anawapongeza wachezaji, benchi la ufundi na viongozi wa timu hiyo.
Timu ya Yanga, viongozi na mashabiki wanatarajiwa kurejea nchini baadaye leo kwa ndege iliyotolewa na serikali, ikiwa ni sehemu ya Rais Samia Suluhu Hassan kuunga mkono timu hiyo iliyokuwa ikiiwakilisha Tanzania katika mashindano ya kimataifa.
Spread the love NAJUA umesikia na unazijua Derby nyingi kutoka jiji la London,...
By Mwandishi WetuSeptember 24, 2023Spread the love USHINDI huu ni wako mteja wa Meridianbet kama mechi...
By Mwandishi WetuSeptember 22, 2023Spread the love ANITWA Pablo Martín Páez Gavira ‘Gavi’, sasa ni mchezaji...
By Mwandishi WetuSeptember 21, 2023Spread the love KAMPUNI ya Bia ya Serengeti Breweries Ltd (SBL) kupitia...
By Mwandishi WetuSeptember 20, 2023
Leave a comment