August 15, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Yanga waiteka Dar, Pitso awavuliwa kofia

Spread the love

 

Klabu ya soka ya Yanga, hii leo tarehe 26 Juni 2022, ilisimamisha jiji la Dar es Salaam, kwa hafla yao ya kusherekea ubingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara, waliokabidhiwa jana jijini Mbeya. Anaripoti Kelvin Mwaipungu…(endelea)

Sherehe hizo zilianza kwenye uwanja wa ndege wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam, majira ya saa tano asubuhi wakitokea jijini Mbeya na kulakiwa na mashabiki sambamba na wanachama wa klabu hiyo waliojitokeza kwa maelfu kwenye uwanja huo wa ndege.

https://www.youtube.com/watch?v=a3vmCXNtJGQ

Msafara wa klabu ya Yanga, ulitoka Uwanjani hapo majira ya saa sita mchana, kwa kupitia Tazara, Kamata mpaka mtaa wa Msimbazi kwenye makao makuu ya watani zao klabu ya Simba.

Hafla hiyo ya ubingwa huo wa 28 zilinogeshwa na uwepo wa basi lililotumika kuwabeba wachezaji sambamba na benchi la ufundi la timu hiyo, na kutumia Saa tatu kutoka uwanja wa ndege hadi makao makuu ya klabu hiyo.

Picha za tukio hilo lilienda mbali kupitia mitandao ya kijamii, kiasi cha kumuibua kocha wa zamani wa Mamelodi ya Afrika Kusini na Ahly ya nchini Misri, Pitso Mosimane ambaye kupitia ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa Twitter aliwapongeza Yanga na kutaka kuwa mfano wa kuigwa.

error: Content is protected !!