May 29, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Yanga waing’ang’ania Simba kileleni

Spread the love

 

BAADA ya kuibuka na ushindi wa mabao 2-0, dhidi ya Jkt Tanzania Yanga sasa inafikisha jumla ya pointi 61, sawa na Simba ambo wapo kileleni. Anaripoti Kelvin Mwaipungu…(endelea)

Mchezo huo wa Ligi Kuu Tanzania Bara ulichezwa kwenye Uwanja wa Jamhuri Jijini Dodoma ambapo Yanga ilifanikiwa na kuondoka napointi tatu wakiwa ugenini.

Yanga imefikisha pointi 61, huku ikiwa mbele kwa michezo minne dhidi Simba ambao bado wapo kileleni wakiwa na michezo 25, huku wakiwa na tofauti ya mabao ya kushinda na kufungwa.

Yacouba Sogne, mshambuliaji wa Yanga

Mabao ya leo kwenye mchezo huo yalifungwa na Yacouba Sogne kwenye dakika 27. mara baada ya kuunganisha krosi ya Kibwana Shomari na bao la pili liliwekwa kambani na Tuisila Kisinda kwenye dakika ya 30

Mara baada ya mchezo huo Yanga itasafiri kuelekea mkoani Shinyanga kwenye mchezo wa robo fainali wa kombe la shirikisho dhidi ya Mwadui Fc ambao wameshuka Ligi Kuu jana mara baada ya kukubali kichapo cha bao 1-0, kutoka kwa Tanzania Prisons.

error: Content is protected !!