November 29, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Yanga waikamua Kagera Sugar, warejea kileleni

Spread the love

KLABU ya Soka la Yanga imeibuka na ushindi mwembamba wa bao 1-0 dhidi ya Kagera Sugar na kurejea kileleni mwa Ligi Kuu Bara kwa kufikisha pointi 23 sawa na Azam FC lakini kukiwa na utofauti wa magoli ya kufunga. Anaripoti Mwandishi Wetu, Mwanza … (endelea).

Katika mchezo huo uliopigwa leo tarehe 13 Novemba, 2022 kwenye dimba la CCM Kirumba jijini Mwanza, ulionekana kuwa mgumu kwa wachezaji wa timu zote mbili kutokana na hali mbaya ya uwanja uliokuwa umejaa maji katika baadhi ya maeneo baada ya mvua kunyesha.

Hata hivyo, Yanga walipata bao la kwanza na la ushindi, dakika ya 18 baada ya kiungo mshambuliaji kinda kutoka timu ya vijana Clement Mzize kuunganisha kwa kichwa krosi iliyochongwa na Feisal Salum.

Bao hilo lilionekana kuwaamsha wachezaji wa Kagera Sugar ambao walipeleka mashambulizi mengi ya hatari langoni mwa Yanga.

Dakika ya 70 Kagera Sugar ambao wameanza kunolewa na Meck Mexime, walipata Penalti baada ya golikipa wa Yanga kumchezea rafu Hamiss Kiiza hata hivyo Erick Mwijage alikosa Penalti iliyopanguliwa na Djugui Diarra.

error: Content is protected !!