June 26, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Yanga wabanwa mbavu nyumbani

Wachezaji wa Yanga wakimdhibiti mshambuliaji wa Etoile du Sahel katika mchezo wao wa leo Taifa

Spread the love

WAWAKILISHI pekee wa michuano ya kimataifa nchini, Yanga leo wameshindwa kuutumia vizuri uwanja wa nyumbani baada ya kulazimishwa sare ya bao 1-1 na Etoile du Sahel ya Tunisia katika mchezo wa kwanza wa hatua ya 16 bora ya Kombe la Shirikisho la Afrika. Anaripoti Erasto Stanslaus … (endelea).

Katika mechi hiyo iliyochezwa kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam ilikuwa na kila aina ya ushindani kutokana na timu kucheza kwa kushambuliana kwa zamu.

Kutokana na matokeo hayo Yanga ili isonge mbele katika michuano hiyo inatakuwa kutoka sare kuanzia mabao 2-2 au kuibuka na ushindi wa aina yoyote katika mchezo wa marudiano utakaochezwa wiki mbili zijazo.

Yanga ndiyo walikuwa wa kwanza kupata bao dakika ya pili ya mchezo huo kwa njia ya penalti lililofungwa na nahodha wa timu hiyo, Nadir Haroub ‘Cannavaro’ baada ya Simon Msuva kuangushwa katika eneo la hatari.

Etoile ambao ni wadeni wa Simba wa fedha za usajili wa mshambuliaji wao, Emmanuel Okwi walipata bao la kusawazisha dakika ya 47 kupitia kwa Ben Amour Amine kwa shuti la mbali linalomshinda kipa Barthez na kutinga wavuni.

 

 

 

error: Content is protected !!