December 8, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Yanga vs Simba, ubabe vs heshima

Wachezaji wa Simba na Yanga wakiingia uwanjani

Spread the love

MCHEZO wa 99 wa watani wa jadi, Simba na Yanga ni mechi ya vita kati ya ubabe na heshima kwa wakongwe hao wa soka nchini Tanzania. Anaandika Erasto Stanslaus … (endelea).

Vita kubwa katika mechi hiyo itakuwa kwa Yanga kutaka kuendeleza ubabe mbele ya Simba, huku Simba wao wakisaka ushindi ili warudishe heshima yao kwa Yanga.

Tangu Ligi Kuu Tanzania Bara ianzishwe mwaka 1965, Simba na Yanga zimekutaka katika michezo 98 ya mechi za ligi hiyo huku Yanga wakiwa wameshinda mara nyingi zaidi ya Simba, hivyo mchezo huo utakuwa na kurudisha heshima au kuendeleza.

Katika mechi hizo 98 Yanga imefanikiwa kuibuka na ushindi katika michezo 34 huku Simba wakiibuka na ushindi katika michezo 30 na kugawana pointi katika mechi 34.

Mechi ya leo itakuwa na ushindani mkubwa sana huku kila timu ikiwa na nia ya kuendeleza ubabe na kurudisha heshima, lakini nafasi walizokuwa nazo timu hizo katika msimamo wa ligi utaongeza ushindani.

Simba inayoshika nafasi ya nne katika msimamo wa ligi hiyo, inahitaji pointi tatu katika mchezo huo ili kupunguza uwiano wa pointi kati yake na Yanga ambao ipo kileleni ikiwa na pointi 31, huku watani wao wakiwa na pointi 23.

Kwa upande wa Yanga wao wanahitaji ushindi katika mchezo huo kwa lengo la kujikita kileleni mwa msimamo wa ligi hiyo, ili kuongeza matumaini ya kurudisha taji lao walilopokwa na Azam FC msimu uliopita.

Simba wataingia uwanjani wakitokea kambini Zanzibar, watakuwa wanategemea nyota wake, Emmanuel Okwi, Jonas Mkude, Ibrahim Ajibu, Ivo Mapunda na Ramadhani Singano.

Yanga wao wanatokea Bagamoyo; wataongozwa na Amisi Tambwe, Mrisho Ngassa, Simon Msuva, Ali Mustapha ‘Bathez’ na Haruna Niyonzima na wengine.

Dakika 90 za mchezo huo ndiyo zitakazoamua, Simba itarudisha heshima yake au Yanga wataendeleza ubabe mbele ya hasimu wake

error: Content is protected !!