June 27, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Yanga, Platnum waingiza 91 mil, kuvaana na Kagera kesho

Nahodha wa Yanga, Haruna Niyonzima akimtoka mchezaji wa FC Platnum katika mechi yao ya kwanza

Spread the love

MCHEZO wa Kombe la Shirikisho Afrika uliozikutanisha timu ya Yanga ya Dar es Salaam dhidi ya FC Platnus ya Zimbabwe iliyochezwa kwenye Uwanja wa Taifa, mwishoni mwa wiki iliyopita imeingiza Sh.91,660,000.

Mechi hiyo ambayo ilimalizika kwa Yanga kuvuna ushindi mnono wa mabao 5-1, ulihudhuliwa na watazamaji 14,563 waliokata tiketi kushuhudia mchezo huo.

Mgawanyo wa mapato katika mchezo huo ni, VAT 18% sh. 13,982,033, Gharama ya tiketi sh. 12,380,000, Uwanja 15% sh. 9,794,694.92, Gharama za mchezo 15% sh. 9,794,694.92, TFF 5% sh. 3,264,898.31, CAF 5% sh. 3,264,898.31 na Young Africans 60% sh.39.178,779.66.

wakati huo huo, Ligi Kuu Tanzania Bara itaendelea kesho (Jumatano) kwa viwanja vitatu kutimua vumbi, Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam Yanga watawakaribisha Kagera Sugar mchezo utakaoanza majira ya saa 10 kamili jioni.

Jijini Tanga maafande wa Mgambo Shooting watakua wenyeji wa Simba SC katika mchezo utakaofanyika uwanja wa Mkwakwani, huku jijini Mbeya wenyeji Mbeya City watawakaribisha timu ya ya Stand United kutoka mkoani Shinyanga kwenye uwanja wa Sokoine.

error: Content is protected !!