July 1, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Yanga ni kimataifa zaidi, yawatupa Wazimbabwe kwao

Mashabiki wa timu ya Yanga

Spread the love

YANGA ni kimataifa zaidi, ndiyo lugha unayoweza kuisema baada ya timu hiyo kusonga mbele katika michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika baada ya kuitupa nje timu ya FC Platnum ya Zimbabwe kwa jumla ya mabao 5-2.

Yanga imefanikiwa kusonga mbele katika michuano hiyo pamoja na kufungwa bao 1-0 katika mchezo wa marudiano uliochezwa kwenye Uwanja wa Mandava uliopo nje kidogo ya jiji la Buyawayo nchini Zimbabwe.

Wawakirishi hao pekee wa michuano ya kimataifa wa Tanzania, wamefanikiwa kusonga mbele katika hatua hiyo ya pili ya michuano hiyo baada ya kuvuna ushindi mnono wa mabao 5-1 katika mechi ya kwanza iliyochezwa kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Yanga sasa itavaana na mshindi kati ya Etoile du Sahel ya Tunisia au Benifica de Luanda ya Angola.

 

error: Content is protected !!