January 28, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Yanga mwendo mdundo, yaipiga JKT 3-1

Mshambuliaji wa Yanga, Danny Mrwanda akipambana na beki wa JKT Ruvu

Spread the love

KLABU ya Yanga imezidi kuchanja mbuga katika mbio za kutwaa ubingwa wa msimu huu, baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 3-1 katika mchezo wake wa 19 dhidi ya JKT Ruvu, uliochezwa kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Kwa ushindi huo, Yanga imefikisha pointi 40 ikiwa kileleni katika msimamo wa Ligi Kuu Bara na kuiacha mpinzani wake mkuu Azam ikiwa nafasi ya pili kwa ikiwa na pointi 36 baada ya kucheza michezo 18. Simba ipo nafasi ya tatu ikiwa na pointi 32 baada ya kucheza mechi 20.

Shukrani kwa mshambuliaji wa Yanga, Simoni Msuva aliyeifungia mabao mawili katika mechi hiyo dakika ya 34 kwa njia ya panalti na lingine dakika ya 57. Bao lingine la Yanga limefungwa na Danny Mrwanda dakika ya 42.

Mabao ya mawili ya Msuba aliyofunga katika mchezo huo, mbali na kuipa Yanga pointi tatu lakini pia imemweka kileleni katika orodha ya wafungaji katika msimu huu, kwa kufikisha mabao 11 akimwacha Mrundi Didier Kavumbagu mwenye mabao 10.

Bao la kufutiwa machozi la JKT Ruvu lilifungwa na Samuel Kamuntu dakika 45.

error: Content is protected !!