Thursday , 2 February 2023
Home Kitengo Michezo Yanga mabingwa Ngao ya Jamii
MichezoTangulizi

Yanga mabingwa Ngao ya Jamii

Spread the love

 

KLABU ya Soka ya Yanga wameibuka kidedea kwa ushindi wa bao 1-0 dhidi ya watani wao Simba Sc na kubeba Ngao ya Jamii ikiwa ni ishara njema kuelekea msimu mpya wa Ligi Kuu Bara 2021/2022. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea)

Katika mchezo huo uliopigwa leo tarehe 25 Septemba 2021 kwenye Uwanja wa Benjamini Mkapa jijini Dar, Yanga waliandika bao lao katika kipindi cha kwanza dakika ya 13 ya mchezo kupitia kwa Fiston Mayele aliyepokea pasi safi kutoka kwa Farid Mussa.

Katika mchezo huo mkali na wa kuvutia Yanga walionekana kutawala zaidi mchezo huo kwa kuonesha soka safi na kuwakosha mashabiki waliokuwa wamefurika ndani ya uwanja huo.

Hata hivyo, katika dakika ya 20 ya mchezo Wekundu wa Msimbazi walipata pigo baada ya mlinzi wao wa kutegemewa, Joash Onyango kujeruhiwa kichwani na mchezaji mwenzie Chriss Mugali wakati wakiwania mpira wa kona. Nafasi ya Onyango imechukuliwa na Kenedy Wilson.

Pia dakika ya 92 ya mchezo, Simba walipata pigo tena baada ya kiungo wao mkata umeme, Injinia Thadeo Lwanga raia wa Uganda kutolewa nje kwa kadi nyekundu baada ya kumfanyia madhambi nyota wa Yanya, Feisal Salum.

Wakizungumza baada ya mchezo huo, mfungaji pekee wa bao hilo, Fiston Mayele raia wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, amesema ushindi huo ni furaha ya kipekee kwao na wanamshukuru Mwenyezi Mungu kwa hatua hiyo.

Naye Nahodha wa timu hiyo, Bakar Nondo Mwamnyeto amesema haikuwa rahisi kupata ushindi huo, lakini imeonesha kubeba Ngao ya Jamii ni dhahiri picha imeonekana kuwa nini kitatokea mbeleni.

“Tuliwaona wenzetu walikuwa vizuri katikari kipindi cha kwanza lakini baada ya Mwalimu wetu kutupatia mbinu tumefanikiwa kuwadhibiti na kuondoka na ushindi,” amesema.

Aidha, Nahodha wa Simba, John Bocco mbali na kuwapongeza Yanga kwa ushindi huo, ametoa wito kwa mashabiki wa Simba kutokata tamaa kwa kuwa hiyo ni sehemu ya mchezo.

Hii ni mara ya sita kwa Yanga kubeba Ngao ya Jamii ambapo mara ya mwisho kunyanyua ndoo hiyo ilikuwa mwaka 2015.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoTangulizi

Mo Dewji achomoza bilionea pekee Afrika Mashariki

Spread the loveMAZINGIRA mazuri ya uwekezaji nchini Tanzania yamezidi kuleta matunda baada...

Habari MchanganyikoTangulizi

Bilioni 213 za miradi ya DMDP zaistawisha Temeke

Spread the loveJUMLA ya Sh bilioni 213 zimetumika kuboresha sekta ya afya,...

Habari za SiasaTangulizi

Dk. Bashiru aibuka na bei za vyakula, “Njaa inadhalilisha nchi”

Spread the loveMBUNGE wa kuteuliwa na Rais, Dk. Bashiru Ally, ameitaka Serikali...

Habari za SiasaTangulizi

Rais Samia ahoji fedha za Plea-Bargaining

Spread the love  RAIS Samia Suluhu Hassan, ameitaka Tume ya kuangalia namna...

error: Content is protected !!