Friday , 3 February 2023
Home Kitengo Michezo Yanga kuzindua Wiki ya Mwananchi Z’bar
Michezo

Yanga kuzindua Wiki ya Mwananchi Z’bar

Mwenyekiti wa kamati ya habari na hamasa wa Yanga, Suma Mwaitenda
Spread the love

 

MABINGWA wa Kihistoria nchini Tanzania, Yanga ya jijini Dar es Salaam itazindua ‘Wiki ya Mwananchi’ Jumapili hii tarehe 22 Agosti 2021, katika Uwanja wa Aman Zanzibar. Anaripoti Wiston Josia na Damas Ndelema, TUDARCo … (endelea).

Pia, wiki hiyo itaadhimishwa nchi nzima kwa wanachama na wapenzi wa timu hiyo kufanya shughuli mbalimbali za kijamii ikiwemo kuchangia damu.

Itahitimishwa Jumapili ya tarehe 29 Agosti 2021, katika Uwanja wa Benjamin Mpaka, Dar es Salaam.

Hayo yamebainishwa na viongozi wa Yanga leo Ijumaa, tarehe 20 Agosti 2021, walipozungumza na waandishi wa habari, makao makuu ya timu hiyo mitaa ya Jangwani na Twiga, Kariakoo jijini Dar es Salaam.

Mwenyekiti wa kamati ya habari na hamasa wa Yanga, Suma Mwaitenda amesema mgeni rasmi kwenye uzinduzi huo kwenye uwanja wa Aman atakuwa Makamu wa Pili wa Rais visiwani humo, Hemed Suleiman Abdulla “ambaye tayari amethibitisha kuhudhuria.”

Amesema, kesho Jumamosi watafanya shughuli mbalimbali visiwani humo ikiwemo kuzindua matawi mawili makubwa.

Suma amesema, siku ya Jumapili asubuhi, wataanza kwa maandamano yatakayoanzia Ofisi Kuu ya Yanga iliyopo Kariakoo kwenda Uwanja wa Aman.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Hemed Suleiman Abdullah

Aidha amesema, watapita nyumbani kwa Fatuma Karume, mjane wa Rais wa kwanza wa Zanzibar, Abeid Aman Karume kumjulia hali, kuzungumza naye kisha kuomba dua ya kumwombea Hayati Abeid kisha safari ya kwenda uwanjani itaanza.

“Wapenzi wa Yanga hii ni shughuli yao na tunawalenga wananchi ambao hawajawai kutuangusha na wao ndiyo wenye shughuli na ndiyo washehereshaji wakubwa,” amesema Suma

“Lazima tuoneshe ukubwa na mkubwa ni mkubwa tu, kwa hiyo wacha tukaoneshe ukubwa wetu. Tunawaomba sana wapenzi wa Yanga na mashabiki kujitokeza kwa wingi wakiwa wamevalia jezi za timu yetu,” amesema

Suma amesema, licha ya wiki hiyo kuzinduliwa Zanzibar lakini shughuli zitakuwa zikiendelea maeneo mbalimbali nchini “hivyo, tuwaombe wananchama na wapenzi wetu kujitokeza kufanya shughuli za kijamii na kuchangia damu hospitalini na viongozi ngazi za huko watatusaidia kuratibu ziezi hili.”

Mwenyekiti huyo wa kamati habari na hamasa amesema, kilele cha wiki hiyo kitafanyika tarehe 29 Agosti 2021, katika Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam ambapo kutafanyika utambulisho wa wachezaji na jezi za msimu ujao 2021/22.

Siku hiyo “tutatambulisha wachezaji wote hata kama mmewaona na nafasi zao, kutambulisha benchi la ufundi na tunaweka utaratibu wa kuzindua jezi za nyumbani na ugenini. Jezi zimekwisha kamilika na ni nzuri sana na za kisasa kabisa.”

Kwa upande wake, Katibu Mkuu wa Yanga, Hajji Mfikirwa amesema, kila jambo huwa linapimwa mwisho “na unaweza kuchelewa jambo lakini pia ukawa mshindi, tunawaomba mashabiki zetu wajitokeze kwa wingi.”

“Mwaka huu kutakuwa na surprise nyingi, tutakuwa tunazindua jezi na kiingilio hakitakuwa kikubwa kwa hiyo tunawanaomba wananchi wajitokeze kwa wingi waje kushuhudia kile ambacho tumewaandalia,” amesema

Amesema, kuna shughuli mbalimbali za kijamii zinaendelea kufanywa mikoani ikiwemo ujenzi wa madarasa “kwa hiyo siku ya kilele yenyewe kutakuwa na watu elfu sitini na watu zaidi ya milioni 50 ya watu wengine duniani watakaofutilia hafla siku hiyo.”

Katibu mkuu huyo amesema, jezi za msimu huu ni bora kulizo za msimu uliopita na kuwaomba mashabiki zao kujiandaa kupata jezi “yenye ubora kabisa na sisi huwa hatubahatishi.”

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Michezo

GGML: Uwanja mpya wa Geita Gold FC kukamilika Mei, 2023

Spread the loveUWANJA wa Magogo unaojengwa na Halmashauri ya Mji wa Geita...

Michezo

Wanafunzi chuo Mwalimu Nyerere wapongezwa kwa ushindi

Spread the love  UONGOZI wa Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere (MNMA)...

Michezo

Arsenal waipopoa Manchester United

Spread the loveKLABU ya Arsenal inayoshiriki Ligi Kuu England imewatandika Mashetani Wekundu...

Michezo

Mchezaji Singida apoteza maisha mazoezini

Spread the love  MCHEZAJI na kapteni wa timu ya vijana ya Singida...

error: Content is protected !!