KOCHA wa Yanga, Cedric Kaze amesema atawakosa wachezaji watano kuelekea mchezo wa leo wa Ligi Kuu Tanzania Bara dhidi ya Coastal Union. Anaripoti kelvin Mwaipungu, Dar es Salaam … (endelea).
Mchezo huo wa mzunguko wa pili utapigwa kwenye Uwanja wa Mkwawani mkoani Tanga ambapo katika kipindi cha miaka mitano Yanga hawajawahi kuibuka na ushindi.
Akiongea na waandishi wa habari Kaze alisema kuwa kwenye mchezo wa leo atawakosa wachezaji watano kutokana na sababu tofauti huku malengo yao ya ushindi yakiendelea kusalia.
“Kwenye mchezo wa leo tutamkosa Mapinduzi Balama ambaye ni majeruhi ya muda mrefu, Carlinhos anatumikia adhabu, Said Ntibanzokiza bado hajapona pia tutamkosa Ditram Nchimbi ambaye aliumia kwenye mazoezi ya jana sambamba na Adeyum Salehe,” alisema Kaze.
Mchezo huo utapigwa majira ya saa 10 jioni huku Coastal Union wakiwa na kumbukumbu ya kupoteza kwa mabao matatu kwenye mchezo wa mzunguko wa kwanza uliopigwa kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam.
Leave a comment